TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749



Kwa wale waliokuwa wakisubiri kwa mda mrefu kauli ya aliyekuwa waziri mkuu Edward Lowasa kusema hadharani na kwa uhakika ni nini dhamila yake juu ya kugombea uraisi wa Tanzania 2015. Leo ameamua kuwaweka mkao wa kula mashabiki na wapinzani wake.
Kupitia ukurasa wake wa facebook, ametangaza rasimi kuwa ni lini hasa atasema rasimi ni nini maamuzi yake kutokana na nguvu anayodai inamsukuma yeye kuchukua fomu ya kugombea ngazi hiyo kubwa ya uongozi nchini.
"Kwa kipindi kirefu sasa nimekuwa nikiombwa na makundi mbalimbali ya vijana, wazee, viongozi wa dini, chama, serikali na hata wananchi wa kawaida kunitaka nitangaze nia ya kuomba ridhaa kwa chama changu, CCM, ili niweze kuteuliwa kukiwakilisha chama kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kwa kipindi chote nimekuwa nikitafakari pamoja na kumuomba Mungu aniongoze kufanya maamuzi sahihi. Mwishoni mwa wiki hii ninatarajia kutoa kauli yangu juu ya jambo hili na nawaomba tuendelee kumuomba Mungu azidi kutupa nguvu na busara ili tuyatende na kufanya yale yampendezayo." Aliandika Lowasa.

0 comments :

 
Top