Familia zaidi ya 200 zimeathirika vibaya huku nyumba 29 wakazi wake wakilazimika kuhama makazi kutokana na mvua kubwa iliyoanza kunyesha mwanzoni mwa mwezi mei huko Zanzibar.
Mvua hiyo inayoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini imesababisha madhara makubwa na kusababisha mafuriko huko Zanzibar hususani maeneo ya Kwahani, Mwanakwerekwe, Tomondo na Kisauni Mtaa wa Ziwa Maboga.
Hata hivyo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amewaahidi waathirika wa mvua hiyo na kusema serikali yake itawapatia misaada wanayostahili ilikuwawezesha kurejea katika maisha yao ya kawaida.
Nae Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Dk. Khalid Salum Mohamed, alisema eneo lililozama huko mwanakwerekwe ambapo shimo kubwa limetokeza na kuhatarisha usalama wa nyumba zilizojengwa katika sehemu hiyo linahitajika kufanyiwa utafiti wa kina ili kupata ufumbuzi wa kudumu
0 comments :
Post a Comment