Mwenyekiti wa Chama cha Demokratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila anatarajia kufungua kesi Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga kuendelea kwa mchakato wa mabadiliko ya Katiba Mpya.
Mchungaji Mtikila amenukuliwa akisema madhumuni ya kufungua kesi hiyo ni mchakato huo kukiuka hatua mbalimbali muhimu wakati wa kuiandaa ikiwamo kutoa elimu kwa wananchi kipi wanatakiwa kukifanya kabla ya kutoa maoni....
“Nakwenda kufungua kesi hiyo, kutaka mchakato huu unaoendelea ufutwe na utupiliwe mbali, tunataka mchakato unaowashirikisha Watanzania wote, walio katika vyama vya siasa,makundi mbalimbali ya kiraia na madhehebu ya dini na wasio na makundi wala madhehebu,” alisema Mtikila
Aliongeza “Nilikuwa kimya najipanga, najua nitashinda sijajua Mwanasheria Mkuu wa Serikali ataniletea mawakili wangapi lakini nitampangua mmoja baada ya mwingine.” Mchungaji Mtikila alisema, endapo majaji wa mahakama hizo watakaoisimamia kesi hawatatenda haki kutokana na matakwa ya Serikali ya CCM atakata rufaa.
Home
»
»Unlabelled
»
MTIKILA KUFUNGUA KESI
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment