TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

Mjini Mombasa nchini Kenya, hali ni tete kufuatia makabiliano makali ya polisi, baada ya maafisa hao kuvamia msikiti wa musa ulioko majengo mjini humo. Polisi imesema ilichukua hatua hiyo baada ya kupata habari kwamba usajili wa vijana kujiunga na kundi la kigaidi la Al shabaab unafanyika ndani ya msikiti huo. Takriban watu zaidi ya 100 walitiwa mbaroni. Watu watatu akiwemo afisa mmoja wa polisi waliuwawa katika makabiliano hayo siku ya jumapili.

0 comments :

 
Top