TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749




MASTAA mbalimbali nchini wakiwemo wanamziki, wanatarajiwa kushiriki kwenye tukio maalum la kukumbukumbu ya mwaka mmoja tokea kifo cha marehemu Albert  Mangwea (Ngwair) litakalofanyika ndani ya ukumbi wa Nyumbani Park (Samakisamaki Sport), Kihonda Morogoro mjini, kesho Jumatano Mei 28 mwaka huu.
Ratibu mtendaji wa tamasha hilo, Kareem Omary “KO”, amesema maandalizi ya tukio hilo litakalokuwa la kila mwaka, limepewa jina la ‘LOVE CONCERT-KUMBUKUMBU YA KIFO CHA ALBERT MANGWEA’
Kareem amewaomba wadau kujitokeza kwa wingi kuunga mkono kwenye tukio hilo kwani litakuwa la kipekee na la aina yake, ambalo pia litatoa fursa nyingi kwa wakazi hao na mikoa ya jirani na watu kutoka nje ya Tanzania ambao wataudhuria.
”Nawaomba wadau kujitokeza kuonesha upendo wa pamoja , kumbukumbu kwa mpendwa wetu kama ilivyo utamaduni wetu” alisema Kareem, na kuongeza kuwa, siku hiyo Watu mbalimbali watapata kupiga picha na mastaa mbalimbali pamoja na mama mzazi wa Mangwea.
Kareem aliwataja wasanii watakaotoa burudani kuwa ni pamoja na, kundi la Wanachemba, wasanii toka morogoro: Afande Sele, Mc Koba, Chris wa Marya, Belle 9, Samir, Zombie, President Mirrow, Jordan wa Dejavu, na wengine wingi.

Kareem alisema Kabla ya show kuanza kutakuwa na kutakuwa na ibada maalumu ikiwemo ya kanisani nay a Nyumbani.

AIdha Kareem aliongeza kuwa katika tukio hilo ambalo lina[ptarajiwa kuaanza majira ya saa 10 hadi saa 12 jioni, wametoa fursa kwa watoto kutoa burudani, ikiwemo ya kuimba na nyinginezo na baadae kuanzia saa 2 hadi majogoo wasanii hao mbalimbali watatawala jukwaa na kudondosha burudani ya nguvu pande za ukumbini.

0 comments :

 
Top