TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

 
Kikosi Cha Brazil Kilichoshuka Dimbani dhidi ya Croatia katika mechi ya ufunguzi kombe la Dunia 2014 katika uwanja wa Sao Paulo ambapo Brazil iliibuka na ushindi wa bao tatu kwa moja.Picha mtandani 
 
Na Yusufu Nuru
 
 
 
Kila baada ya miaka minne dunia inashuhudia mashindano makubwa yenye historia na heshma ulimwenguni kote ambapo washiriki wa michuano hii wanaonyesha  vipaji na ufundi wao kwa ajili ya kuwaburudisha watazamaji wa mchezo huu maarufu  na wenye mashabiki wengi zaidi.
 
Mapema june 12,2014 fainali za kombe la dunia  2014 zimefunguliwa nchini Brazil, yako matukio muhimu ya kukumbukwa na wanahistoria pamoja na wapenda soka duniani kote.
 
Ni fainali zilizogubikwa na vurugu, maandamano ya wananchi wa kawaida pamoja na wafanyakazi katika mashirika mbalimbali nchini humo wakikipinga michuano hiyo kutokana kwamba zinagharimu mabilioni ya fedha ambazo zingetumika kuboresha huduma za kijamii pamoja na kuongeza mishahara kwa wafanyakazi katika sekta mbalimbali za maendeleo.
 
Vuguvugu la kupinga kufanyika fainali za kombe la dunia zilizua shaka kwa shirikisho la soka duniani FIFA kutokana na matukio kadhaa yaliyosababisha majeruhi na baadhi ya vifo vya raia wa nchi hiyo.
 
Ikumbukwe kuwa wakati Brazil ikiendelea kuandaa miundombinu kwa ajili ya michuano hiyo mataifa mengi ya magharibi(Ulaya) yalikosoa namna viwanja  na miundombinu mingine ilivyokuwa ikiendelea huku uwasi wasi juu ya uwepo wa usalama kwa washiriki ukitajwa kuwa ni hafifu.
 
Hata hivyo matarajio wa wabrazil yamekuwa ni kutwaa ubingwa huo kwa mara ya sita  na kushirkiria recodi kwa muda ambapo Uhispania ndiye bingwa mtetezi baada ya kutwaa ubingwa huo mwaka 2010 katika fainali za kombe la dunia zilizofanyika nchini Afrika ya Kusini.
 
 Mara baada  ya MJAPANI Yuichi Nishimura kupuliza kipyenga macho ya wengi yalikuwa yakimtafuta mshambuliaji wa clabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Brazil Neymar mwenye umri wa miaka 22 kuona anafanya juu chini kupicha bao la mapema kabla ya wageni Croatia.
 
Huzuni ilitanda kwa muda mara baada ya Marcelo wa Brazil kujifunga goli la mapema kabisa na kuifanya Croatia kuongoza kwa bao moja katika kipindi cha kwanza.
 
Ahueni kwa timu ya Brazil ilionekana baada ya mshambuaji Neymar kupachika bao la kwanza akipokea pasi kutoka kwa Oscar  na  kuwatia nguvu mashabiki waliojaa nje na ndani ya uwanja wa Sao Paulo pamoja na wachezaji wenzake wakati wa kipindi  cha  kwanza cha mtanange huo muhimu.
 
Mpaka kipenga cha mwisho Brazil walifanikiwa kuichapa  timu ya Croatia mabao matatu kwa moja ambapo kipindi cha pili Neymar aliongeza bao lake pili kwa mkwaju wa penati ambayo ilizua mjadala miongoni wa watalaamu na wachambuzi wa soka kwa kile wengi walichokiita ni upendeleo kwa wenyeji wa michuano hiyo yenye hisia duniani.Na bao la tatu lilifungwa na kiuongo wa clabu ya Chelsea Oscar Dos Santos baada ya  kuwatoka  mabeki wa Croatia.
 
Kusema  ukweli Brazil hawakuonyesha kiwango cha kutisha kiasi kwamba wanaweza kupambana na timu kubwa kama vile Ujerumani , Uhispania ,Italia ,na Mexico ambazo pia zinatarajiwa kufanya vizuri katika mashindano hayo makubwa duniani.
 
Safu ya ulinzi ya timu ya Brazil ilionekana kuwa na madhaifu pale wapinzani waliposhambulia kwa nguvu huku wachezaji wachache wakionyesha kiwango cha hali ya juu kama vile Neymar, Daniel Alves,Luiz Gustavo ,Thiago Silva ,Bernard na Oscar ambaye alikuwa mchezaji bora katika mechi hiyo ya ufunguzi.
 
Wachambuzi wa soka wanasema endapo Brazil itaendelea kucheza kwa kiwango kama kile walichokionyesha katika mechi ya ufunguzi huenda wakaaga mapema mashindano hayo kutokana  na timu zingine kuwa na wachezaji wazuri .
 
Ushindi wa bao tatu kwa moja umewapa nguvu wabrrazil wa kuendelea kupambana na hata kufikiria kuinyang'anya Uhispania ubingwa.Lakini huu ni mwanzo mzuri kwa Brazil pamoja na kuwepo kwa lawama nyingi zinazomhusu mwamuzi wa mtanange huo kutoka JAPAN kwa mara ya kwanza.
 
Endelea kuwa nasi katika kuifutilia Brazil
ambao ni wenyeji wa fainali za kombe la
Dunia.
 
 
 
 
 
 
 
 

0 comments :

 
Top