Dar es Salaam. Wakati mashabiki wa Yanga, wakimsubirli kwa hamu ujio wa kocha Marcio Maximo, tayari Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuph Manji ametumia zaidi ya Sh690.1 milioni kuwalipa makocha saba waliopitia mikononi mwake tangu 2007 hadi sasa.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na gazeti hiliMwananchi umebaini pamoja na Manji kutumia kiasi cha Sh690.1 milioni wakati Yanga imefanikiwa kuingiza Sh265 milioni ikiwa ni zawadi za Ligi Kuu Bara kipindi cha misimu saba iliyopita.
Manji tangu awe mfadhili alikuwa akitoa fedha nyingi kulipa
makocha kuanzia mshahara na hata wanapovunja mikataba amekuwa akibeba
dhamana ya kulipa fidia na kati ya makocha hao saba waliopitia mikononi
mwake ni Brandts pekee aliyeondoka kwa amani bila kusikia anadai fidia.
Katika makocha hao wote ni Pluijm pekee ndiye aliyeongoza kwa kuchukua mshahara mkubwa kwa mwezi akipokea Sh18 milioni, akifuatiwa na Brandts aliyekuwa akilipwa Sh 17.6 milioni, Tom Santifiet alilipwa Sh12 milioni, Papic Sh 7.5 milioni, Spaso Sh1.2 milioni wakati mshahara wa Timbe haukuwekwa wazi.
Papic alivuna Sh 60 milioni kwa miezi minane ya kwanza aliyoifundisha timu hiyo, lakini aliporudi alikaa miezi minne tu na kutimuliwa hivyo kuambulia kulipwa Ssh 7.5 milioni kama mshahara wa mwezi mmoja na huku akidai malimbikizo ya mshahara wa miezi mitatu kiasi cha dola 15,000 ambazo ni sawa na Ssh 22.5 milioni.
Kocha huyo aliamua kulipeleka suala hilo kwenye Shirikisho la Soka Duniani a( Fifa) na hivyo Yanga kuamuriwa kumlipa kabla haijapewa adhabu.
Kocha mwingine aliyevuna pesa nyingi ni Brandts
aliyeondoka na kitita cha Ssh 211.2 milioni kwa miezi 12 aliyokaa
Jangwani, wakati Pluijm alivuna Ssh 108 milioni kwa miezi sita ya
mkataba wake, huku akiondoka na kuidai Yanga Ssh18 milioni kama mshahara
wake wa mwezi mmoja kwa madai
Yanga ilitaka aondoke wakati alikuwa bado ana mkataba.
Yanga ilitaka aondoke wakati alikuwa bado ana mkataba.
Dusan Kondic yeye alivuna Sh 70.8 milioni kwa
miezi 18 aliyoifundisha timu, lakini aliondoka huku akiidai fidia ya
kuvunja mkataba wake Sh15 milioni na kulifikisha suala hilo Fifa na
hivyo Yanga kuamuariwa kumlipa la sivyo ingeshushwa daraja.
dic alikuja na msaidizi wake Spaso ambaye, yeye alivuna Sh 14 milioni ukiwa ni mshahara wake wa miezi 11 aliyoitumikia Yanga, hata hivyo walivyotimuliwa aliibuka na kusema anaidai fidia ya dola 6,000 ikiwa ni sawa na Ssh 9 milioni kama mshahara wake wa miezi sita iliyobaki.
Kama kuna kocha aliyejuta kuifahamu Yanga basi ni
Tom Santifiet, wengi walipenda kumwuita ‘mtakatifu Tom’., Mbelgiji huyo
alidumu ndani ya timu hiyo kwa siku 80 tu kabla ya kuvunjwa kwa mkataba
wake. A
Kocha huyo alivuna Sh36 milioni kama mshahara wake wa miezi mitatu aliyoinoa timu hiyo, lakini alipovunjiwa mkataba aliibuka na kuidai fidia ya dola 12, 500 sawa na Sh 18 milioni.
Pia, Mganda Timbwe pamoja na mafanikio yake ya
muda mfupi bado alitimuliwa hivyo kuidai Yanga fidia ya dola 53,000 sawa
na Sh 90 milioni.
Mbali na makocha hao Yanga pia imepata hasara ya Sh 416.5 kwa kuvunja mikataba ya watumishi wake ambao ni aliyekuwa katibu wa klabu hiyo Celestine Mwesigwa, aliyekuwa msemaji wake Louis Sendeu, mwanasheria Godwin &Company Advocates na wachezaji wake Steven Marashi na Wisdom Ndlovu.
Chanzo Mwananchi
0 comments :
Post a Comment