TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

Kundi la wanamgambo la Al Shabaab limemtaja kiongozi woa mpya baada ya aliyekuwa mwanzilishi wa kundi hilo Ahmed Godane kuuawa katika shambulizi lililofanywa na majeshi ya Marekani wiki jana.
Kiongozi huyo mpya ni Ahmad Umar ambaye hajulikani sana. Mmoja wa makomanda wa Al Shabaab Abu Mohammed, alisema uamuzi wa kumteua kiongozi huyo ulifikiwa bila pingamizi.
Kundi hilo lilitoa tangazo lao kupitia kwenye mtandao wakiahidi kulipiza kisasi mauaji ya Ahmed Godane.
Maafisa wakuu nchini Somalia awali walitoa taarifa ya tahadhari wakionya dhidi ya mashambulizi ya kulipiza kisasi kutoka kwa kundi hilo.
Al Shabaab wameahidi kulipiza kisasi mauaji ya Ahmed Godane
Tahadhari hiyo ilitolewa huku Marekani ikithibitisha kifo cha Godane kilichotokea kufutia shambulizi la angani lililofanywa na wanajeshi wa Marekani Jumatatu usiku wiki jana.

Msemaji wa Alshabaab amesema kuwa wapiganaji wengine wawili wa kundi hilo pia walifariki katika shambulizi hilo ,yapata kilomita 170 Kusini ya mji mkuu wa Mogadishu .
Katika taarifa yao,kundi hilo lilionya :"kulipiza kisasi mauaji ya kiongozi wetu ni jukumu letu ambalo hatutawahi kukoksa kutekeleza licha ya muda.''
Kwa ruhusa ya Mwenyezi Mungu , bila shaka mtaonjeshwa makali ya adhabu ya milichokifanya.
Tangazo la kiongozi huyo mpya llitolewa dakika chahe tu baada ya kundi hilo kuthibitisha kifo cha Godane.
Mapema JUmapili, waziri wa usalama wa ndani, alisema kuwa seriklali ilipokea taarifa za kundi hilo kupanga kushambulia vituo vya afya, el;imu na taasisi zengine za serikali nchini humo.

0 comments :

 
Top