TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

Wakuu wa vyama vya upinzani UKAWA
Wakuu wa vyama vya upinzani UKAWA

Madhumuni ya mkutano huo ni kueleza msimamo wa UKAWA kuhusu yalioafikiwa katika mazungumzo kati ya viongozi wa vyama vya kisiasa vinavyoundwa kile kinachojulikana kama Kituo cha Demokrasia Tanzania na Rais jakaya Kikwete kuhusu mkwamo uliojitokeza baada ya Ukawa kujitoa kwenye Bunge la katiba. Msimamo wa ukawa unafuatia maelezo yaliotolewa jana na Mwenyekiti wa Kituo hicho mbunge John Cheyo kuhusu matokeo ya mkutano wao na Rais Kikwe

Akizungumza na DW Katibu wa UKAWA Mtatilo amesema kuwa wao msimamao wao wanazingatia yale waliyokubaliana na Rais kwa sababu hakuna mda wa kutosha wa kupitisha maoni na kuelekea na uchaguzi lasivyo inabidi uchaguzi usitishwe na kupisha kupitishwa kwa uchaguzi mkuu.
 Aliongeza kuwa Bunge maalumu linatakiwa kusitishwa ili kupisha maandalizi ya uchaguzi mkuu na kuepussha upotezaji wa fedha za wananchi kwa kuwa baada ya uchaguzi kutakuwa na muendelezo wa uundwaji wa katiba mpya.

Pia alisema kuwa kati ya makubaliano waliyo kubalianan na Rais ni kurekebisha katiba iliyopo ikiwa na mambo kadhaa kama tume huru ya uchaguzi, mgombea huru, matokeo ya urais kuweza kupingwa mahakamani, rais kushinda kwa zaidi ya asilimia 50 na kuwepo kwa kipengele kitakachotoa ruhusa ya kuendelea kujadili kwa katiba mpya baada kupatikana kwa serikali mpya mwaka 2015 kwa kutumia rasimu ya Jaji Warioba.

0 comments :

 
Top