TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

Makamu wa Kwanza wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibari (SUK) amewalipua viongozi watatu wa vyama vya upinzani.
Amewalaumu viongozi hao kwa kugoma kuahirishwa kwa bunge la KATIBA kama miongoni mwa masharti yaliyofikiwa na viongozi wa vyama vya upinzani kabla ya kukutana na Rais Kikwette juzi
."Nimepata taarifa kuwa licha ya viongozi wa vyama vya upinzani wanaounda Umoja wa katiba ya wananchi UKAWA pamoja na kituo cha Demokrasia TCD kukutana Jumapili kwa saa 6:00 na kufikia makubaliano ya nini cha kwenda kuzungumza na Rais Kikwette, viongozi wenzao waligoma kusaini hati ya makubaliano iliyokuwa ikidai kuhairishwa kwa Bunge maalumu la KATIBA."
Alisema baada ya viongozi wa upinzani kukutani na Rais Kikwete mjini Dodoma mara ya kwanza kulitokea kutoelewana kwa viongozi wa vyama vya upinzani na Rais Kikwette alitoa nafasi ya viongozo hao kukutana na kukubaliana nini kifanyike ili kuondoa tofauti zilizopo.
Baada ya kuketi kwa mara ya pili juzina kukubaliana mambo kadhaa viongozi hao watatu Mrema, Cheyo, na dovutwa waligoma kusaini hati ya makubaliano.
"Walipinga kuahirishwa kwa bunge maalumu la Katiba hivyo wamekwenda kuzungumza na Rais Kikwette wakiwa vipande vipande, hakuna katiba mpya itakayopatikana."

0 comments :

 
Top