TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749



Kila gari la kibiashara linaposajiliwa hupewa plate namba yake ya kibiashara ili iwerahisi katika kukusanya mapato ya kodi ya gari lenye namba husika, kwakuwa namba hizo ndiyo kitambulisho cha gari lenyewe.
Ni ajabu kuziona  gari za biashara na zenyeusajili wa kufanya biashara zikiwa na Plate namba aina moja. kitu ambacho hakileti mantiki akilini.
Maswali ya kujiuliza, ni jinsi gani mamlaka husika inakusanya kodi kutoka kwenye hizi gari...? Je kama ni bahati mbaya si wangezigundua tu...?
"Uchumi unaohujumiwa kila kona lazima utadumaa tu. Inawezekana vipi magari haya yawe na namba moja ya usajili? Mapato ya gari moja yanaenda wapi? Haya ni magari ya abiria,, huko kwenye magari binafsi lipo tatizo kubwa!" Hii ni post ya Mtanzania mmoja facebook.
Hii inamaanisha kuwa lazima gari moja halipeleki mapato sehemu husika na kama halipeleki sehemu husika lazima kutakuwa na mwenye mamlaka sehemu husika anajipatia hizo pesa ili gari hili liendelee kupeta.
Je ni nani...?
Kwa macho yangu hii ni mara ya pili naona gari zikiwa na namba moja. Hii inaonyesha ni jinsi gani huu mchezo mchafu umekithili hapa nchini kwetu.
HII NDIO NCHI YETU WATANZANIA NA NINYI NDIO WENYE MAAMUZI NAYO

0 comments :

 
Top