TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

Cloudsfm Radio's photo.
Rwanda imeorodheshwa kuwa nchi ya 7 duniani kwa kutoa huduma za haraka na rahisi za serikali. Ripoti iliyotolewa na baraza la Uchumi duniani imeiorodhesha Rwanda mbele ya Malaysia, Uswisi na Luxembourg ambazo zilichukua nafasi za 8, 9 na 10. Utafiti wa baraza hilo pia umeonesha kuwa serikali ya Qatar ndio iliyo na utendaji bora zaidi ikifuatiwa na Singapore na Finland.



Akiongea na waandishi wa habari mkurugenzi wa Bodi ya utawala ya Rwanda Bwana Anastase Shyaka amesema nchi yake inafanya juhudi kubwa kukuza uwazi na uwajibikaji kwenye mfumo wake, na raia wengi wana habari kuhusu jinsi serikali inavyofanya kazi na kutoa maamuzi. Kwingineko barani Afrika Mauritius iko kwenye nafasi ya 26 na kama Afrika Kusini iko katika nafasi ya 32 Tanzania Je?

0 comments :

 
Top