
Kwa mujibu wa Guinness World Records, Mkongwe 'Mahashta Mûrasi' ni mtu aliyeishi muda mrefu tangia historia ya binadamu, alizaliwa mwaka 1835, Kwa sasa ana umri wa miaka 179.
Mahashta Mûrasi wa India anayedai alizaliwa mwaka 1835. Sio tu ni kuwa ni mtu mkogwe duniani lakini pia mtu aliyeishi muda mrefu tangia historia ya binadamu.
Kwa mujibu wa WorldNewsDailyReport.com nyaraka zote zilizoidhinishwa kumtambulisha huyu mtu zinakubaliana na madai haya.
Mahashta kwa sasa ni mtu aliye kata tamaa ya kufa kwakuwa anaona watu wa karibu yake wanapotea lakini yeye bado anaendelea kuishi, kitu kinachomfanya aamini kuwa kifo huwa kinamkwepa.
"wajukuu zangu wamekufa miaka kadhaa iliyopita, Kwa hili, kifo kimenisahau. Na sasa nimepoteza matumaini yote ya kufa tena!" Alisema Mahashta.
Maofisa wa India wanasema mzee huyo alizaliwa kwenye nyumba moja huko Bangalore, mwezi wa kwanza tarehe 6, 1835 na kutoka 1903, aliishi Varanasi, amako alifanya kazi hadi mnamo mwaka 1957, hadi mwaka wake wa kustafu kazini akiwa na umri wa miaka 122.
0 comments :
Post a Comment