Msanii MYSTORY kwa mara ya kwanza anaenda kuachia wimbo wake alomshirikisha rapa wa kike anayefanya vizuri hapa bongo anayekwenda kwa jina la MYSELF a.k.a CHEMICAL ambaye nae anatamba na kibao chake cha SIELEWI alichomshirikisha SOPRANO pamoja na msanii Yuzo kutoka EAST COAST ambae nae alipata kufahamika kupitia wimbo wa KING CRAZY GK wa baraka au laana jina la wimbo ni NAJIULIZA.
"Kwanza niseme tu kwamba ni wimbo wa rapu niliofanya chini ya prodyuza bonny breezy na nachoweza kusema ni kuwa watanzania inabidi waelewe kilichoimbwa ndani kwa sababu ndo maisha halisi ya mtanzania. Kingine nachoweza nikajivunia ni kuwa colabo nimefanya na watu wanaojielewa na recognition kidogo Chemical ni msanii mzuri Yuzo nae so i think itakuwa poa" alisema Mystory.
Wimbo huo unategemewa kuachiwa kwenye blogs mbalimbali nchini na jumatatu utakuwa tayri ukichezwa redio mbalimbali hivyo basi watanzania tunasubiri kusapoti kilicho chema. Mbali na muziki lakini pia ni mwanachuo wa chuo kikuu cha Dar es salaam ( mass communication) nani anasema muziki na shule hauendi hahaha maneno yake Mystory. Anapatikana kwa social networks zifuatazo INSTAGRAM @ mystorytz FACEBOOK-MAISTORY MC kila la heri kaka.

0 comments :
Post a Comment