TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749


Na Kachero Mbobezi.
Kinachofanywa na CCM katika harakati hizi za Kampeni dhidi ya Mgombea wa Urais wa Umoja wa Vyama vya Ukawa Mh Edward Ngoyai Lowassa si cha Kiungwana na ni hujuma za wazi na makusudi.
Tuongolee eneo la Mabango.
Siku tatu Nyuma Vijana waliojitolea wa Chadema na Marafiki wa Lowassa wakiongozwa na kundi la 4u Movement wanaounda umoja wa marafiki wa Ukawa waliendesha zoezi la kubandika Mabango ya Mgombea wa Urais kupitia Vyama Vya Ukawa Mh Edward Ngoyai  Lowassa.
Katika zoezi hili lililoanza majira ya saa za jioni kwa Mkoa wa Dar es Salaam lilionesha dhahiri kiu ya Watanzania katika kuelekea mabadiliko wanayoyataka,lilionesha kuchokwa kwa Chama Tawala cha CCM.
Makundi Mbalimbali ya Bodaboda, Bajaji, Daladala, Mama Ntilie, Madereva tax,watu binafsi, Machinga na Wafanyabiashara wa kati wenye maduka  walionekana kujitokeza kwa wingi kuyachukuwa mabango haya na kuyabandika kwa hiari yao kwenye maeneo yao na kwenye Vyombo vyao vya usafiri na wengine kuyagombea wakidai hayatofika maeneo wanapoishi, eneo maarufu la kituo cha  bajaji Mwenge,Mwananyamala A,Ujiji,Kinondoni,Tandika,Manzese,Msasani,Kariokoo na Sinza Africasana ni moja ya maeneo yaliyobandikwa mabango haya kwa wingi na muda mfupi tangu kuanza kwa zoezi.
Tofauti na Chama Tawala Juu ya Mgombea wao, ambao wao wenyewe wametumia makampuni binafsi ya Matangazo kufanya kazi hii ya kubandika Mabango ya Mgombea wao,Makampuni kama Outdoor 1,Billboard n.k ni moja ya Makampuni yaliyopewa kazi na CCM kuhakikisha wanabandika Mabango ya Mgombea wao mkoa Mzima.
Cha kufurahisha katika zoezi hili la Marafiki wa Ukawa ni pale zoezi zima lilipokuwa likifanyika, watu wengi walionesha kiu na uhitaji wa Mabango haya kwa kuwa yalichelewa tofauti na Mabango ya CCM ambayo yametapakaa Mji mzima,wananchi walionesha kuwa na furaha na wengi kufikia kuyashangilia na kushangilia, Wakiimba Rais,Rais Rais,Jembe,Jembe, na wengine wakisema huyu ndiye tunayemtaka.
Eneo la Mfano ni Kariakoo ambapo wakati zoezi la kuwekwa kwa Bango kubwa la Mh Edward Lowassa ulijitokeza umati mkubwa wa wafanyabiashara na wananchi wa kawaida na kuanza kuimba Rais,Rais,Rais,Kiboko ya Makufuli na wengine kukejeli Mabango ya CCM.
Umati Mwingine ulishuhudiwa eneo la Manzeshe,Tandale na Tandika Sokoni.
Lakini cha Kusikitisha Mabango haya yameanza kuchanwa na kuondolewa kwa hila na kundi la Vijana waliopewa kazi hii na CCM kwa malipo ya Tsh 10,000,zoezi linaloratibiwa na kusimamiwa na Wagombea Ubunge wa CCM kwenye majimbo ya Mkoa huu kwa agizo maalumu kutoka ngazi za Juu,Shame.
Hii yote ni kiwewe cha Uoga na udhaifu wa mbinu za Mapambano kisiasa na kushindwa kwa siasa za kistaarabu na kisayansi kinachofanywa na chama cha Mapinduzi,CCM.
Mabango mengi maeneo ya Kinondoni,Mwananyamala na Mwenge yameshuhudiwa kuchanwa na kuondolewa siku moja baada ya Kubandikwa.
Siasa za Kizamani na za Kishamba, kuchana Mabango ya Mgombea wa Upinzani.
Kivuli tu Kinaogopewa hivi hivi je Muhisika mwenyewe?
Hakika Edward Ngoyai Lowassa anawanyima Usingizi Viongozi na Mgombea wa CCM.
Ni Rai yangu kuwaomba Viongozi wa CCM kuacha tabia hii chafu na Mbaya inayoendelea kuwachafua na kuwatia Machungu Malofa na Wapumbavu wengi wenye Vichinjio  waliodhamiria kuiondoa Madarakani kwa sanduku la Kura hapo itakapotimu Tarehe 25 October mwaka huu.
Najiuliza je na wao wakiamua kuyabandua na kuyaondoa Mabango  Mengi ya CCM waliyoyabandika kwa gharama kubwa kutakalika?
Tuache hizi siasa Nyepesi Nyepesi na zenye kuashiria Vitendo vya Chuki na Uvunjifu wa Amani.
Salaam.
Kachero Mbobezi.

0 comments :

 
Top