Mgombea ubunge jimbo la Segerea, Julius Mtatiro, kupitia UKAWA kwa tiketi ya CUF, leo ameeleza jinsi pesa za wananchi jimbo la Segerea na kata kwa ujumla zinavyoliwa na viongozi wa CCM, ambazo zilitakiwa kushughulikia matatizo sugu ndani ya kata ya Kipawa yanayowakumba wananchi.
Alieleza kuwa kata ya kipawa inasumbuliwa na matatizo ya miundombinu, kama vile barabara ya ngo'mbe, tatizo la ukosekanaji wa maji, ukosekananji wa hospitli ya kata pamoja na miundo mbinu ya shule zilizopo katika kata hiyo.
Ameyaeleza hayo alipokuwa akihutubia umati wa wananchi waliojijtokeza kusikiliza sera zake katika kata ya Kipawa jimbo la Segerea mkoa wa Dar es salaam. Alieleza kuwa kunakiasi kikubwa sana ambacho wananchi wamekuwa wakizurumiwa kwa kuliwa na viongozi wa CCM jimbo na kata, kitu ambacho kitakomeshwa yeye atakapokuwa mbunge endapo wananchi watamchagua.
Alisema kuwa jimbo la Segerea linaingiza mapato zaidi ya bilioni 50 na hupewa bilioni 50 kutoka katika bajeti kila mwaka na kufanya kuwa na bilioni 100 ambazo zinatakiwa kushughulikia matatizo yanayo wakumba wananchi kama vile ujenzi wa soko, matatizo ya huduma za afya, maji na tatizo la miundombinu ya elimu kama vile shule. Alifafanua kuwa ilitakiwa kila kata kwa jimbo la Segerea kupata milioni 500 kutokana na mgao huo wa mapato.
Lakini pia alieleza kuwa kila mwaka ilitakiwa kutengwa pesa kutoka kwenye mapato ya jimbo kiasi cha asilimia 5 kwa wakina mama na asilimia 5 kwa vijana kwaajili ya mikopo yenye riba na mashariti nafuu ili kutatua matatizo ya ajira. Alieleza kuwa kwa jimbo lake ilitakiwa kutengwa milioni 100 kwaajili ya mikopo hiyo na anasikitika kwa wannchi kutopata mikopo ya namna hiyo.
"Hizo pesa zinaliwa na viongozi wa CCM ambao ndio walikuwa kwenye vikao vya almashauli. kwa mfano Jerry Slaa amekuwa diwani na meya wa ilala mwenye mshahara wa kawaida tu, lakini kwa sasa anajengo ghorofa ambayo hata mimi siwezi kujenga wakati mimi namzidi uwezo wa kuingiza kipato kwa mwezi kutokana na shughuli zangu za hapa na pale. Je amepata wapi hizo pesa kijana mdogo kama yule." alisema Mtatiro.
Kwa upande wake mgombea udiwani wa kata hiyo kupitia UKAWA, Kennedy Thomas, alisema kuwa yeye atakuwa mstari wa mbele kusikiliza kero za wananchi kwa kuwa karibu nao, lakini pia kuwa bega kwa bega na mbunge kuhakikisha wanavisimamia vyema vipaumbele vya jimbo lao.
Alisema kuwa anasikitika kuona miundombinu ya barabara kutokuwa mizuri kiasi cha kuwake madimbwi mvua ikinyesha na hata kusababisha maji kuingia kwenye makazi ya wananchi wa kata ya kipawa.
Lakini pia wanawake kupata tabu ya kutafuta maji huku na kule huku pia huduma za matibabu zikiwa ni kero kwao wakati wanatakiwa kuondokana na matatizo hzyo kwani uwezo upo kinachokosekana ni viongozi makini wa kusimamia na kuwa na dhamira madhubuti ya kuleta mabadiriko katika jamii, na UKAWA imekusudia kufanya yote hayo endapo wananchi wataipa ridhaa ya kuwachagua viongozi wote wa UKAWA , kuanzia udiwani, ubunge na urais.
Mtatiro ni kati ya wabunge wa UKAWA wanaofanya kampeni za nyumba kwa nyumba kuanzia asubuhi hadi jioni kila anapofanya mikutano katika kila kata.

0 comments :
Post a Comment