TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

Mtatiro akiwa na mgombea udiwani kata ya Minazi mirefu, Kassimu Mshamu 

Mgommbea ubunge wa jimbo la Segerea kupita UKAWA kwa tiketi ya CUF, Julius Mtatiro amevunja ngome ya CCM kwa jimbo la Segerea kwa kufanya mkutano mkubwa ambao uliudhuliwa na wafuasi na wananchi wengi kusikiliza sera zake, huku wakizunguka naye nyumba kwa nyumba kata nzima.
Mkutano huo ulifanyia katika kata ya Minazi mirefu jimbo la Segerea akipokuwa akizindua kampeni za udiwani kata hiyo ambapo walinadi sera zao huku waelezea matatizo mbalimmbali yanayowakabili wananchi wa kata hiyo, waliyodai kuwa yamesabbishwa na serikali ya CCM.
Mtatiro ametoa vipaumbele vyake kumi kwa wananchi wa jimbo la Segerea, ambavyo ni, kuanzisha ofisi ya mbunge ambayoitakuwa ni sehemu ya kusikilizia kero za wannchi, kuhakikisha fedha za miradi ya maendelea (400 milioni) zinaifikia kila kata, udoreshaji wa miundombinu, kushughulikia tatizo la maji kwa kufufua visima, kuhuisha miundombinu na machinjio ya Vingunguti, kujenga nchi mpya kwenye kata zisizo na shule,kuboresha sekta ya afya, kusimamia michezo kwa uthabiti, kutengeneza mifuko ya kuweka na kukopa katika kila kata(kutoka katika sehemu ya mshahara wa mbunge na michago), kupigania haki za wananchi kwa ujumla.
Kwa upande wake diwani wa kata hiyo ya Minazi mirefu Kassim Mshamu, ameahidi ushughulikia matatizo matatu sugu kwa wananchi wa kata ya Minazi mirefu, miundombinu, tatizo la kutokuwa na shule, pamoja na kukosekana kwa zahanati kwa kata hiyo.
Ameeleza kuwa wananchi wanahitaji mabadiriko na si ushabiki wa vyama na hivyo wachague UKAWA kwani CCM imesababisha maumivu makubwa saana kwa wananchi wa kata hiyo kwa muda mrefu na sasa wanahitaji kupata ahueni ya kimaisha.
Hata hivyo wananchi walionyesha kuchokwa na mfumo wa serikali iliyopita kwani hakuna ilichowaanyia mpaka sasa huku wakiwa na raslimali nyingi saana zinawazunguka ambazo ni mtaji kwa maendeleo ya kata yao.
Mtatiro akiongea na madereva wa bodaboda wa kataya Minazi mirefu

Mtatiro akipita nyumba kwa nyumba na mgombea udiwani Kaissim



Wananchi wakisikiliza sera

Kada wa CCM akichana kadi ya CCM na kujiunga na CHADEMA


Mtatiro na Kassim wakionyesha wakitembea na wannchi kuelekea ofisi za CUF kata ya minazi mirefu



0 comments :

 
Top