Tangazo la Serikali Na. 294 la tarehe 27/7/2015 chini ya kifungu cha 124A cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343, ukurasa wa 5 kifungu 2.1(k) kinasema:-
“Viongozi wa vyama vya siasa, wagombea au wafuasi wao wahakikishe kuwa majengo wanayotumia kufanya kampeni sio ya Ibada. Vile vile, vyama vya siasa vihakikishe kuwa havitumii viongozi wa dini kupiga kampeni kwa ajili ya vyama vya siasa au wagombea wao”.
Lakini katika maadili hayo hayo, ukurasa wa 7, kifungu 2.2(i) kinasema:-
“Vyama vya siasa au Wagombea hawaruhusiwi kuomba kupigiwa kura
kwa misingi ya UDINI, UKABILA, JINSIA AU RANGI.”
Ni wazi kampeni za Lowasa zinatakiwa zisitishwe mara moja, kazi ya kiongozi ni kuunganisha watu na sio kuwatenganisha, kesho wakiibuka pentekoste, Sabato, angalikana nao wakisema wanataka rais wao tutafika!!!!!!!?
👆👆👆👆👆
Tunaomba hatua ichukuliwe baina ya Ukawa/Chadema na Lowassa kwa ujumla maana amevunja kanuni za uchaguzi.
Ikibidi hata sisi tulipigie kelele.
Kanuni zimetungwa ili zifanye kazi.
0 comments :
Post a Comment