KAFULILA AMLIPUA WARIOBA&JK HOT MIX
Na Kilawa the Iron
Akihojiwa kwenye kipindi cha Hot mix ndani ya EA TV kuhusu uamuzi wa
Warioba na baadhi ya viongozi wanaojipambanua kama wazalendo kuzunguka
nchi nzima kumpinga Lowasa kuhusu ufisadi husan wa richmond , mbunge
huyo alijibu;
"Kwanza watanzania waelewe kwamba kabla Lowasa hajapokewa alihojiwa kuhusu hili, na kwa mara ya kwanza aliweza kumhusisha JK na sakata hili kwa kiwango cha kutosha".
"Kwanza watanzania waelewe kwamba kabla Lowasa hajapokewa alihojiwa kuhusu hili, na kwa mara ya kwanza aliweza kumhusisha JK na sakata hili kwa kiwango cha kutosha".
Kwa mfano, wakati nchi ikiwa kwenye msukosuko wa kusubiri mitambo ya
richmond, JK alitua nchini kutoka marekani na kuzungumza na wanahabari
na kuwapoza watanzania kwamba ametoka marekani na amekutana na wamiliki
wa richmond na wamemuhakikishia kwamba siku chache mitambo ingetua
nchini.
Swali la kujiuliza , Kamati ya Mwakyembe ilisema ilichunguza mpaka
marekani hakuna mahala kampuni hiyo ilisajiliwa marekani, je Mhe Rais
alikutana na nani marekani? Tumwamini Rais au Kamati ua Mwakyembe?.
Alihoji Kafulila
Akisisitiza hoja yake, Kafulila alieleza kwamba maelezo ya Lowasa kwa
umma kuwa alitaka kuvunja mkataba wa richmond mapema lakini Katibu Mkuu
wizara ya fedha Mgonja wakati huo na Mwanasheria mkuu wa serikali
Mwanyika wakati huo walisisitiza kuwa mamlaka za juu zilikataa bado
haijakanushwa popote na Mgonja, Mwanyika, Rais mwenyewe na hata
wasaidizi wake wa chama na serikali mpaka sasa. Hii inathibitisha kwamba
aliebeba kampuni hii feki ni Mhe Rais Mwenyewe bila kupepesa maneno.
Aidha ukifuatilia maneno ya Mhe Mwakyembe bungeni kwamba yapo mambo
walificha kulinda heshima ya serikali, unaweza kujiongeza tu, kama
yaliyosemwa yalitosha Waziri mkuu kama mkuu wa serikali bungeni
kuanguka, yaliofichwa yangemwangusha nani kama sio Rais?
Pamoja na hayo, Kafulila alisisitiza kwamba watanzania wakumbuke
kwamba hasara pekee iliyopatikana katika sakata la richmond ni serikali
kuipa zabuni kampuni feki na hivyo nchi kuchelewa kupata umeme kwasababu
ilishindwa kuzalisha. Lakini serikali kama serikali haikulipa senti
moja kwa kampuni hiyo kwakuwa haikutekeleza mkataba. Hii ni tofauti na
masakata mengine kama ya mabehewa feki ambapo zabuni ilipewa bila
kufanyiwa uchunguzi kama ilivokuwa richmond na bado na ikalipwa zaidi
ya 230bn..na bado hatuoni uwajibikaji. Alisema Kafulila.
Kuhusu warioba na wengine wanaojiita wazalendo kumpinga Lowasa
kwenye kampeni, Kafulila alisema Warioba anaweza kumpinga Lowasa kama
mwana ccm lakini sio kama mzalendo kwani hana uhalali wa kuvaa viatu vya
uadilifu wakati anahusishwa kwenye tuhuma za ufisadi wa bilioni 6 kupitia
scandal ya Mwananchi Gold zilizothibitishwa na PCCB na kupelekwa kwa DPP
kwajili ya mashtaka kufikishwa mahakamani ingawa mpaka sasa zimekuwepo
taarifa za Mhe Rais kuzuia DPP kufikisha mashtaka hayo mahakamani. Hivyo
Warioba akienda kwenye kampeni ajiandae na hayo pia. Maana tunaambiwa
ufisadi wa Lowasa lakini hakuna mahala uchunguzi wa chombo chochote
kilichothibitisha baada ya kufanyia kazi kama ilivyo kwa warioba ambapo
pccb imefanyia kazi na kubaini ukweli.
Kafulila alisema hata Sumaye alipokewa UKAWA ni mtu safi kwani hakuna
mahala katika orodha ya matukio ya ufisadi wa awamu ya Mkapa utakuta
jina la Sumaye. Na hapa ikumbukwe awamu hii ilikuwa na orodha ndefu ya
matukio ya ufisadi kuliko awamu zote katika utawala wa nchi hii
ikifuatiwa na awamu ya Kikwete. Alisema kuwa katika matukio mengi
mawaziri wa mkapa na hata mkapa mwenyewe alihusishwa katika wizi
akitolea mfano wa ufisadi wa mgodi wa KIWIRA. lakini hakuna tukio lolote
utamkuta Sumaye wakati yeye ndio alikuwa msimamizi mkuu wa serikali.
Pamoja na kueleza kuhusu mafanikio ya jimbo kama mbunge na nafasi ya
UKAWA katika uchaguzi huu ambao vyombo vya kimataifa kama ICC
vinafuatilia kwa karibu. Kafulila alisisitiza uchaguzi wa amani, na
kutaka makamanda wa jeshi la polisi kupuuza maelekezo ya kisiasa
yanayotolewa na wanasiasa kuanzia ngazi ya taifa mpaka mikoa na wilaya
ambapo kuna wakuu wa mikoa na wilaya ambao ni wanasiasa lakini wanamlaka
juu ya ma RPC na OCD Kwa maelezo kwamba maangamizi ya raia
yatakapotokea watakaowajibishwa ni waliofanya mamuzi na sio hao
walioelekeza kwa simu
0 comments :
Post a Comment