TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749




MGOMBEA ubunge jimbo la Segerela kupitia CUF anayeungwa mkono na vyama vyote vinavyounda UKAWA, Julius Mtatiro, amezidi kusisitiza kuwa wananchi wanatakiwa kutatuliwa kero zao na mbunge wao kwa kuwasikiliza, kuwafuata waliko na kuwapa majibu sahihi ya matatizo yao na kuyatatua.
Ameeleza kuwa njia pekee ya kufanya hivyo ni kutumia mfumo wa siku 2 + siku 1 + siku 2, yaani katika siku tano za kazi katika wiki, yeye atazigawa kwa kutenga siku mbili kuwa ofisini kusikiliza wananchi watakaokuwa na shida naye, siku moja ya kutembelea wananchi jimboni kwake na siku mbili zingine ni kutumikia wananchi kitaifa.
Ameyasema hayo katika mkutano uliofanyika kata ya Kipawa jimbo la Segerea jijini Dar es salaam. Pia amewataka wananchi wa jimbo la Segerea kutambua kuwa yeye ndiye mgombea aliyeteuliwa na kupitishwa na UKAWA kugombea ubunge jimbo la Segerea, ingawa NEC imefanya hujuma za kutomtoa mgombea wa CHADEMA katika karatasi ya kupigia kura, wakati hagombei, ili tu kuleta mkanganyiko kwa wapiga kura na kupunguza kura kwa UKAWA.
“Kwakuwa mnaimani na UKAWA, mimi Julius Mtatiro ndiye niliychaguliwa kupeperusha bendera ya UKAWA kupitia CUF, na mwenzangu wa CHADEMA yeye alijitoa katika nafasi ya kugombea ubunge kwa jimbo la Segerea na kuniunga mkono mimi. Kwahiyo mnatakiwa kuiachana na mgombea wa CHADEMA kwani mkimchagua mtakuwa mmeharibu kura zenu, yeye sio mgombea, mimi ndiye ninatakiwa kuungwa mkono na wanachama wote wa CHADEMA, CUF, NCCR MAGEUZI na NLD”
Amezidi kufafanua kuwa kwa upande wa urais ni mzee wa maamuzi magumu kupitia CHADEMA, Edward Lowassa ndiye anapeperusha bendera ya UKAWA na ndiye anatakiwa kuungwa mkono na vyama vyote vya CUF, CHADEMA, NCCR MAGEUZI, na NLD, ili kuleta mabadiriko


Mtatiro akitoa elimu ya jinsi ya kupiga kura kwa wananchi wa jimbo la Segerea
Vijana wa bodaboda wakisikiliza sera za Mtatiro na diwani wa kata ya kipawa Kennedy, katika harakati za mtaa kwa mtaa
Mama mjasilia mali akielimishwa jinsi ya kupiga kura na kupewa sera za jinsi gani atatatuliwa kero zake kama mfanya biashara mdogo
Mama ntilie nao hajawaacha, anawafuata kila sehemu na kuwasikiliza na wao wanamsikiliza na kupata elimu ya jinsi ya kupiga kura

Vijana ndio tegemeo la UKAWA
Wajasilia mali wakionyesha kazi zao na kusikiliza nini atawafanyia yeye kama mbunge na rais wa UKAWA, Lowassa

0 comments :

 
Top