DC Arusha, Kenani Kihongosi, kwa kushirikiana na jeshi la polisi wamemkamata askari polisi aliyekuwa anaiba umeme wa TANESCO ambao alijiunganishia kinyemela.
Baada ya kumpekua nyumba anayoishi na gari yake, alikutwa na viroba vya konyagi, kete za bangi, gongo na vyuma mbalimbali.
"Kupitia ofisi ya Mkuu wa Wilaya Arusha, nilipata taarifa za uwepo wa baadhi ya wananchi wanaofanya hujuma ya kuiba umeme, kama kiongozi mwenye dhamana niliwasiliana na jeshi la polisi, na tulikwenda kwenye nyumba moja ambayo taarifa zake zilinifikia" Kenani Kihongosi, DC Arusha
"Tumemkamata mmiliki wa nyumba ambayo ilikuwa inaiba umeme, mwenye nyumba huyo ni askari na amekiri kuiba umeme tangu Septemba mwaka 2019, jambo hilo kama kiongozi wa serikali limenisikitisha, kwa kuwa askari ni wasimamizi na wanalinda sheria" Mhe. Kenani Kihongosi, DC Arusha
"Niliomba upekuzi ufanyike nyumba nzima, baada ya upekuzi kukapatikana viroba vya konyagi ambavyo serikali ilishapiga marufuku, pia tulikuta vyuma mbalimbali vinavyotumika katika miradi ya serikali, kete za bangi, gongo, madumu ya Petroli na dizeli" Kenani Kihongosi, DC Arusha
"Tutaendelea na operesheni ya kuwasaka na kuwakamata wanouhujumu kwa kuiba umeme wa TANESCO bila kumuangalia usoni mtu yeyote. Nawaomba watu wote wa jiji la Arusha wafuate sheria na kuwa wazalendo kwani kuhujumu ni moja ya dalili ya kukosa uzalendo" Kenani Kihongosi, DC Arusha.
0 comments :
Post a Comment