Dkt. Festo John Lugange, Naibu Waziri TAMISEMI, Jumanne ya tarehe 05 January 2021 amefika Jimboni Segerea na kuona maendeleo ya ujenzi wa stendi ya Kinyerezi unaojumuisha barabara ya Kinyerezi - Limbanga - Ulongoni - Gongolamboto. Mheshimiwa Naibu Waziri ameona pia maendeleo ya ujenzi wa madaraja ya Ulongoni A na B
Katika ziara hii, Mh. Naibu Waziri amepata maelezo juu ya mkakati wa kudumu wa serikali wa kujenga kingo za mto Msimbazi ambako kwa mjibu wa Mratibu wa mradi wa DMDP Mkoa wa Dar Es Salaam, Eng. Ndyamkama Tayari benki ya dunia imetenga kiasi cha dola za marekani milioni Mia Moja kumi na nne (114M US dollars) Kwa ajili ya ujenzi wa kingo hizo.
Ujenzi huu utajumuisha daraja la Jangwani ambapo mradi unatarajiwa kuanza mwezi Machi mwaka huu 2021. Mhandisi Ndyamkama, ameeleza kuwa tayari baadhi ya mito inayoelekeza maji yake Msimbazi imeanza kujengwa akiitaja mito ya Ng'ombe, Tenge na mita zaidi ya mia tatu (300m) kutoka kwenye madaraja ya Ulongoni A na B ambako Mheshimiwa Naibu Waziri ameshuhudia ujenzi wake unaoendelea.
Akizungumza katika ziara hii, Mbunge wa Jimbo la Segerea, Mh. Bonnah Ladislaus Kamoli amemueleza Mh. Naibu Waziri juu ya adha ambazo wananchi wanazipata kutokana na Mto huu. Amesema pamoja na mpango mzuri ambao serikali inao, kunapaswa kufanyika juhudi za makusudi tena za uharaka huku akisisitiza kuwa hii ni ahadi ya Mh. Rais kipindi cha Kampeni.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mh. Ng'wilabuzu Ludigija amemshuku Mh. Naibu Waziri kwa kufika kwake na kuona maendeleo ya mradi huo huko akiishukuru Serikali ya awamu ya tano chini ya Mh. John Joseph Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuhakikisha inatimiza dhamira yake ya kuwaondolea adha watanzania.
0 comments :
Post a Comment