TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749


Na Thadei Ole Mushi.

Kosa amefanya Gigy Money, adhabu wanapewa watu wengine. 

Ningekuwa pale TCRA Cha Kwanza ningelitaka jeshi la Polisi kumkamata Gigy na baadaye tungemtoza faini ya Milioni 100 au aozee hapo Segera. Angezitafuta Hadi achakae hili lingekuwa funzo kwa wengine wote wenye wehu kama wa Gigy Money kujifunza. 

Baadaye nikifikiria Sana naagiza waliokuwa wanarusha lile tamasha Live wakamtwe wakaguliwe vyeti, ikiwezekana wapimwe na mkojo kabisa.... waunganishwe kwenye Kesi na wengine wangejifunza.

Hii ingesaidia kuokoa haya mamilioni ya Shilingi ambayo Chibu ameyawekeza hapa. Naamini mfanyakazi wako akifanya Kosa anayetakiwa awe wa kwanza kuadhibiwa ni Mhusika kulingana na MAADILI ya kazi yake. 

Kama Amber Ruth alifanya zaidi ya Gigy Money na tukamalizana naye inakuwaje tunaua hii TV hivi hivi ambayo inatusaida kupunguza tatizo la Ajira kwa vijana wetu huko mtaani?

Miezi sita ni mingi Sana nawawazia vijana walioajiriwa hapa wanaishije kwa Miezi sita, naziwazia familia zao, naiwazia Kodi ya Serikali iliyokuwa inalipwa na wasafi.

Wengi wametoa maoni ya kuwalalamikia TCRA, wanaua ndoto za uwekezaji kabisa nchini. 

Tukio lilikuwa Live mtu kavuta Bangi yake kaamua kuonyesha Uchi wake Wasafi wangelifanyaje hapo? Tukidili na Gigy itamsaidia sana.... Hakuna mwingine atarudia.

Anyway mm naamini Kama tatizo likianzia kichwani lazima litakuja kuonekana hadharani tu. Tushauriane Sana na akili zetu kabla ya kutoa maamuzi. Yanaumiza Sana.

Kuanzia Kesho wafanyakazi wote wa wasafi wakiamka wanapiga mswaki wanarudi kulala.

Naomba kuwa Tofauti hapa.

Ole Mushi
0712702602

0 comments :

 
Top