Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Ubungo jijini Dar Es
Salaam nchini Tanzania, kinakusudia kuwasilisha mashtaka kwa Tume ya
Haki za Binadamu na Utawala Bora dhidi ya jeshi la polisi mkoa wa
Kinondoni na Kanda Maalum ya Dar Es Salaam kwa kuzuia mkutano wake wa
hadhara uliokuwa ufanyike jana Julai 21.
Aidha, mashtaka hayo yatahusu pia kutaka uchunguzi juu ya polisi
kulipua bomu linalodaiwa kuwa la ‘machozi’ wakiwa katika gari yao
katika eneo alilokuwepo mbunge John Mnyika akifanya mazungumzo na
askari hao, bomu ambalo lilimkosa mbunge huyo na kwenda kumjeruhi
mwananchi mwingine aliyekuwa nje ya duka jirani na eneo la tukio.
Taarifa iliyotolewa na chama hicho jimbo la Ubungo ambayo East Africa
Radio inayo nakala yake inasema kuwa itawasilisha mashtaka hayo kwa
mujibu wa katiba ya nchi ibara ya 130 (b) kifungu kidogo (c) na Sheria
ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kifungu cha 15.
Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Ubungo jijini Dar Es
Salaam nchini Tanzania, kinakusudia kuwasilisha mashtaka kwa Tume ya
Haki za Binadamu na Utawala Bora dhidi ya jeshi la polisi mkoa wa
Kinondoni na Kanda Maalum ya Dar Es Salaam kwa kuzuia mkutano wake wa
hadhara uliokuwa ufanyike jana Julai 21.
Aidha, mashtaka hayo yatahusu pia kutaka uchunguzi juu ya polisi
kulipua bomu linalodaiwa kuwa la ‘machozi’ wakiwa katika gari yao
katika eneo alilokuwepo mbunge John Mnyika akifanya mazungumzo na askari hao, bomu ambalo lilimkosa mbunge huyo na kwenda kumjeruhi mwananchi mwingine aliyekuwa nje ya duka jirani na eneo la tukio.
Taarifa iliyotolewa na chama hicho jimbo la Ubungo ambayo East Africa Radio inayo nakala yake inasema kuwa itawasilisha mashtaka hayo kwa mujibu wa katiba ya nchi ibara ya 130 (b) kifungu kidogo (c) na Sheria ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kifungu cha 15.

0 comments :
Post a Comment