TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

JESHI la Polisi kanda maalumu ya Dar  es salaam limekanusha taarifa iliyotolewa na Chama Cha Demacrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwa bomu limemkosakosa mbunge wa CHADEMA Bwana JOHN MNYIKA alipokuwa akihutubia wananchi wa Maeneo ya Mabibo.
Taarifa hiyo ilitolewa na Kamishina wa Polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam Ally Mnege alipokuwa akiongea na  waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam.
Mlege alisema askari hawakulipua bomu kwenye mkutono huo, bali askari mwenye namba E5340 D/CPL. Julius, alikuwa akisogeza boksi lenye mabomu ya machozi y akurusha kwa mkono ndani ya gari ndipo ukatokea msuguano wa mabomu hayo na kusababisha bomu dogo kulipuka ndani ya gari
Aliendelea kufafanua kuwa askari hao walikuwa kwenye doria za kawaida ndipo wakawa wanapita karibu na mkutano huo.
Pia alisema kuwa hakuna aliyekuwa amedhulika na mlipuko huo.

0 comments :

 
Top