HATIMAYE mwenyekiti wa Chama Cha Democrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freman Mbowe jana amewasilisha kwa maandishi ushahidi wake makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es salaam.
Maelezo ambayo yamewasilishwa yamekuwa siri nzito kwani yanatokana na msimamo wa CHADEMA kudai wanaushahidi na tukio la mauaji ya mlipuko wa mabomu lililotokea Juni 15 mwaka huu Mkoani Arusha.
Maelezo hayo yaliwasilishwa na wakili wa Mbowe Peter Kibatala . Kibatala alisema kuwa maelezo hayo yalipokelewa na Mkuu wa idara ya upelelezi (CID) Kamishina Advocate Nyombi.
Baada ya kuwasilisha maelezo hayo Wakili Kibatala likataakuzungumzia yaliyomo ndani
"Nathibitiisha bila shaka, nimewasilsha majibu kwa niaba ya Mbowe leo(Jana) makao makuu ya Polisi kama tulivyo kubaliana. Lakini yaliyoandikwa humo ni siri...siwezi kuzijadili, tusubili kutoka kwao", alisema Kibatala
Hatua ya kuwasilisha ushahidi huo kimaandishi, ilifikiwa jumatano ya wiki hii katika mahojiano baina ya Polisi na Mbowe .
siku hiyo Mbowe aligoma kuwasilishaushahidi wake Polisi kama alivyyotakiwa kwenye barua aliyoandikiwa na Jeshi la Polisi Julai 17 mwaka huu, kwa kile alichosema hadi Rais Jakaya Kikwete atakapounda tume ya kijaji kuchunguza tukio hilo.
Katika barua hiyo Mbowe alitakiwa apeleke ushahidi huo na asipopeleka kunaadhabu aliyo eleza kuwa atapatiwa ikiwa ni kifungo cha jela miaka mitatu au faini ya SH 500,
000.
Home
»
»Unlabelled
»
CHADEMA WAWASILISHA POLISI USHAHIDI WA MAUAJI YA ARUSHA
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment