TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749



Na GODWIN SIKAJULA (SJMC), DAR ES SALAAM

WANANCHI wa Kigamboni wameulalamikia uongozi wa mamlaka ya vitambulisho vya Taifa Tanzania NIDA, kwa utaratibu mbovu juu ya zoezi zima la upigaji picha za vitambulisho vya Taifa.

Malalamiko hayo yametolewa jana katika ofisi za NIDA zilizoko Kigamboni ambako zoezi la upigaji picha lilipamgwa kufanyika kwa wananchi waishio, Tungi, Vijibweni, Kigamboni, Mjimwema, Somanjila, Kimbiji, Kisarawe, Pemba mnazi, na Kibada.

Wakitoa malalamiko yao wanchi hao walieleza kuwa, mwanzo kila mtu alikuwa anapiga picha katika ofisi za kata yake, lakini mnamo tarehe 22 Julai mwaka huu zoezi hilo lilisitishwa na kuwataka Wananchi kwenda moja kwa moja katika ofisi za NIDA Kigamboni na ndiko watakako piga picha hizo.

“Tulipo kuja hapa NIDA wakatuambia tuje tarehe 29 Julai ambayo ndiyo leo, lakini chakushangaza tumefika hapa tangu asubuhi hakuna  zoezi lolote linalo endelea wakati sisi tumefunga shughuli zetu na kuna wengine ni Wanafunzi wamesafiri kutoka mikoani, na majibu yao wao wanasema tuondoke hadi tutakapo pigiwa simu”, alisema Pascal Faustine.

Akizidi kueleza juu ya mfumo mzima wa pale, mmoja wa wananchi Peter Amos alisema hakuna utaratibu maalumu wa kuwaeleza Wananchi nini cha kufanya zaidi ya kuulizana wao wenyewe.

Kwa upande mwingine viongozi waliopo katika ofisi za NIDA walikataa kuzungumzia malalamiko hayo hadi alipo tafutwa kwa njia ya simu Afisa habari wa NIDA William Thomas na kuzungunzua jambo hilo.

“Zoezi linaendelea na litazidi kuendelea, isipokuwa kutokana na uwingi wa watu hatuwezi kuwahudumia watu zaidi ya 1000 na ndio maana tukaamua kwamba, tutatoa majina ya kila mtu na tarehe ya kuja kupiga picha hizo ili kuwa na watu wachache tunaoweza kuwahudumia”, alusema Thomas.

0 comments :

 
Top