Rais
Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na maofisa waandamizi wa
Wizara ya pamoja na wajumbe wa Chama cha Makampuni ya Simu za mkononi
alipokutana nao kwa mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 23,
2013.PICHA NA IKULU
RAIS wa jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mh Jakaya Mlisho Kikwete ameagiza Wizara za Serikaki zinahusika na kodi na mawasiliano pamoja na makampuni ya simu za mikononi nchini, kukutana maramoja kutafuta jinsi gani ya kumaliza mvutano wa kodi mpya ya kadi za simu hizo za mikononi.
Rais Kikwete amesema hayo Jumanne alipokutana na viongozi wa Wizara ya Fedha, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Tekinolojia na wawakilishi wa makampuni ya simu ya TTCL, Airtel, Vodacom, Tigo, na Zantel katika kikao cha pamoja kilichofanyika Ikulu Dar es salaam
"Nawaombeni kaeni pamoja, wekeni mbongo zenu pamoja, wekeni akili zenu pamoja, tutafute namna gani tunaweza kujaza pengo hili la Sh Bilioni 178 endapo tutakubaliana kuwa kodi hii inawabebesha mzigo mzito na kuwa pengine menejimenti ya kodi yenyewe ni ngumu", alisema Rais Kikwete
Rais Kikwete alieleza kuwa, ni vigumu kutengua fedha zote hizo kwani zilishapitishwa na Bunge na tayari ziko kwenye bajeti ya matumizi ya mwaka 2013/2014.
Home
»
»Unlabelled
»
RAIS KIKWETE ATOA KAULI YAKE JUU YA KODI YA 1000 YA LAINI YA SIM
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)

0 comments :
Post a Comment