TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

                                      
Jeshi la Polisi mkoani Dar es Salaam limefanikiwa kumkamata askari bandia wa kikosi cha usalama wa barabarani (Pichani) akiwa amevalia sare za trafiki akiendelea na kazi pasipo kugundulika kwa siku kadhaa.

Trafiki huyo bandia mwenye cheo cha Sajint alikamatwa na Polisi akiwa "kazini" maeneo ya Tabata Kinyerezi akiwa amevaa sare mpya za Askari wa Usalama barabarani, kikoti cha kuakisi mwanga, kofia nyeupe huku akiwa ameshika kitabu cha kutoza faini (Notification) kwa madereva wanaopatikana na makosa ya kukiuka sheria za usalama barabarani.

0 comments :

 
Top