TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaamu, wamesema kuwa wamejipanga vyema katika ulinzi kwa kipindi chote cha sikukuu ya Eid El-ftri, lengo ni kuhakikisha wananchi wa Dar es salaam wanasheherkea sherehe hiyo kwa amani.
yalisemwa hayo na  Kamanda wa jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Suleiman Kava, alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam
Pia Kova alipiga marufuku disco toto na kusema kuwa watakao endesha disco hizo watakamatwa kwakuwa huwa maranyingi husababisha maafa kwa watoto.
alizidi kuonya wale wote waliokusudia kufanya vurugu za aina yoyote ile katika maeneo hasa ya ufukweni, bar, club na hata wanao endesha vyombo vya moto huku wakiwa wamelewa.
Aliongeza kuwa mwaka huu jeshila polisi limeimarisha zaidi kitengo cha ulinzi kwani maeneo ya fukwe za bahari kutakuwa na vituo vya polisi vya mda ambavyo vinaahamishika, lengo ikiwa ni kurahisisha upokeaji wa malalamiko kwa yeyote atakaefanyiwa vitendo vibaya.
Katika kuhakikisha ulinzi unafanikiwa zaidi, Kova alisema jeshi la polisi litatumia vikosi vya maji, kikosi cha anga, mbwa, makachero pamoja na farasi.
Akitoa uthibitisho wa jinsi jeshi la polisi lilivyo jipanga aliisema kuwa msako wa kuwakamata waarifu umeanza mapema, ambapo mpaka sasa wamekamatwa watuhumiwa 172.

0 comments :

 
Top