MBUNGE wa
kuteuliwa, James Mbatia (NCCR-Mageuzi), ameibua madudu mapya katika
sekta ya elimu, ambao umebaini kwamba kwenye mitihani ya majaribio ya
darasa la saba, baadhi ya maswali ya kuchagua, hayakuwa na majibu.
Mitihani hiyo ya
majaribio ya programu maalum ya matokeo makubwa sasa, kwa mujibu wa
Mbatia ilifanywa na wanafunzi wa darasa la saba hivi karibuni katika
masomo ya Hisabati, Kiswahili na Kiingereza katika wilaya 40 nchini.
Katika uozo huo
ambao ameutaja kama kuwakatisha tamaa wanafunzi katika somo la Hisabati,
Mbatia alisema maswali sita yalibainishwa na wataalamu wa Hesabu kuwa
hayana majibu huku swali moja likiwashinda maprofesa waliofanya mtihani huo.
Alisema katika swali moja, namba 33 walimu wa hisabati katika shule kubwa za msingi walishindwa kulifanya na baadaye kubainika kuwa ni swali la mwanafunzi anayechukua fani ya uhandisi katika vyuo vya elimu ya juu.
Mabatia alisema
katika mitihani hiyo, kunamakosa mbalimbali ya lugha pamoja na usahihi
wa masuala mbalimbali, ikiwemo programu hiyo kuainishwa kama matokeo
makubwa sasa huku jina la wizara likiandikwa Wizara ya Elimu na Mafunzo
ya Ufundi Stadi.
Alisema katika
mtihani huo wa hisabati,ambao wanafunzi wa darasa la saba walitakiwa
kufanya kwa saa mbili, mtaalamu wa aligebra aliufanya kwa saa 2:10 na
profesa saa 2:03 huku yeye akifanya kwa saa 2:19.
“Matokeo haya ni
kuwakatisha tamaa na kuwaua wanafunzi kabla ya kufanya mitihani, ni
lazima hatua madhubuti zichukuliwe kuokoa mapigo haya ya moyo wa Taifa
ambayo yakizimika, Taifa linakufa,” alisema.
Mbatia alitoa
mapendekezo yake ili kuokoa janga hili la elimu ikiwa ni pamoja na
kuundwa kwa Tume ya Kudumu ya Elimu, itakayoshughulikia kuhakikisha
ubora wa elimu nchini. Tume hiyo kwa mujibu wa Mbatia, inatakiwa kuwa na
mamlaka ya kuhakiki utendaji wa taasisi mbalimbali za elimu, ambazo
hadi sasa zimeonekana kutotimiza vyema wajibu wake.
“Ninaamini
kwamba,tume hiyo itakapoundwa itasaidia kubainisha wazi nini falsafa na
malengo hasa ya utoaji wa elimu nchini, kulingana na wakati tulionao,
jambo ambalo halitakuwa geni kwani katika uongozi wa awamu ya kwanza,
kulitungwa falsafa na miongozo mbalimbali,”alisema
Alisema kwa
mamlaka aliyonayo Rais na na kwa mujibu wa katiba na kwa kadri anavyoona
inafaa, anaweza kuunda tume na kuipatia majukumu ya utendaji stahiki,
ikiwemo kutoa idhini ya matumizi ya mitaala mingine.
Pia alipendekeza
tume hiyo ihariri na kupitia vitabu vya kiada kwa shule nchini na
kufanya utafiti za kisayansi kuhusu masuala mbalimbali ya elimu kwa
lengo la kuinua ubora wa elimu.
Akizungumza na
gazeti hili, Msemaji wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bunyanzu
Ntambi alikiri kuwa jinala wizara limekosewa katika mitihani hiyo.
Alipoulizwa kuhusu uozo uliopo katika mitihani hiyo ya majaribio,
alisema atafuatilia na atatoa taarifa kwa gazeti hili baadaye.
HabariLeo
Home
»
»Unlabelled
»
MBATIA AIBUA MADUDU MAPYA MTIHANI WA DARASA LA 7
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment