Sheikh Ponda amejeruhiwa na risasi leo jioni akiwa mkoani morogoro .
Dhahama hiyo imempata baada ya kushuka kwenye taxi ambako kulikuwa leo
akiendesha mhadhala baada ya mhadhala huo kukawa kama kuna maandamano
kueleke barabarani, gafla polisi walitokea na kuanzanza kutawanya wakati
huo yeye alikuwa hayupo.
Ndipo mda mdogo akawasili akashuka na ndipo akapigwa risasi.
RPC, Faustine Shilogile, anasema hali ni shwari
ila Ponda hajui hali yake Maana polisi walizuia gari la Ponda wamkamate,
lakini wananchi wakaanza kushambulia polisi ndipo wakarusha risasi
hewani kutawanya watu, lakini wananchi wakamtorosha. Anasema taarifa ni
nyingi za uongo, hakuna watu polisi wala hospitali waliozingira na
anaomba anayejua alipo atoe taarifa
(Shuhuda):
---------------

By
Zantsan
Kweli nimeshindwa kuamini kilichotoke, sheikh
ponda kubigwa risasi. Nilikuwepo pale uwanjani tena nilikuja mapema
kabisa na hivyo kushuhudia kila kitu kilichotokea.
Kimsingi sikuona sababu ya Sheikh Ponda kutokewa na tukio baya kiasi
kileambacho hakionyeshi ubinaadamu kabisa, utu wetu, uhuru wetu na hata
heshima tuliyonayo watanzania kwenye jumuia za kimataifa. Mpaka sasa haieleweki ni nani hasa kampiga risasi Sheikh Ponda, lakini minong'ono ya watu wanasema ni polisi wamehusika.
Binafsi pamoja na kufuatilia kwa ukaribu sikuona ilikotokea risasi
hata aliyepiga na nilikuwa mbali kidogo na tukio. Ila nilimwona wakati
anapandishwa kwenye pikipiki akiwa tayari amekwisha kupigwa risasi.
Imewahuzunisha wengi!
Jamaa ameongea kwa muda mfupi sana ni takribani dakika 18, kwani alianza
kuongea saa 11:54 na alimaliza kuongea saa 12:12 jioni. Hali ya
uwanjani kwakweli ilikuwa shwari sana, hata polisi hawakuonekana jirani
walikuwa kwa nyuma kabisa huku wakiwa wamejisheheni kwa zana zote za
kazi.
Mara baada ya ponda kukaribia kumaliza kuongea alisema kuwa muda
hautoshi isipokuwa ilitangaza kuwa kesho baada ya swala ya adhuhuri
atakuwa kwenye msikiti wa mkoa wa morogoro wa Boma road ambapo ataongea
kwa kirefu hivyo kuwataka waislamu kesho kuhudhuria Boma road.
Inavyooneka polisi walipanga wamkamate hata kabla ya kuongea katika ule
mkutano na ndio maana walitega sehemu kana kwamba walikuwa wakimsubiri
aingie wamkate. Lakini katika hali isiyotarajiwa na wengi Sheikh Ponda
iliingia uwanjani kupitia upande wa pili ambapo msafara wake ulikuwa na
gari moja tu na taksi mbayambaya kiasi kwamba wala huwezi kudhania.
Mara tunashangaa gari imesimaa na Sheikh Ponda na Amiri wa wahadhiri
Tanzania Sheikh Kondo Bungo wakashuka,wakapita kwenye kundi la waislam
kwa nyuma ghafla kivumo cha shangwe na Takbir kikavuma huku umati wa
waislam waliohudhuria hapo ukiitia allahu akbar, allahu akbar nk.
Wakati huu jukwaani alikuwa akiongea Sheikh Said Riko na ndio
aliyewapokea kwa kuanzisha takbir ambayo iliitikiwa na waislam allahu
akbari,allahu akbar, allahu akbar. Kwa sababu waliingia kwa kuchelewa
ilibidi mara moja Sheikh Said Rico ampishe sheikh Kondo Bungo,amir wa
wahadhiri Tanzania aongee. Wakati anaendelea kuongea kabla hata
hajamaliza umeme ukakatika, likachukuliwa jenerata ambalo lilikuwa
jirani likawashwa, na muhadhara ukaendelea kama kawaida. Sheikh Kondo
Bungo akamaliza mada yake, akarudi Sheikh Said Riko, akaongea na
kuchangisha michango kwa ajili ya kuendeleza harakati kwa muda wa kama
dakika tano hivi ndipo akaruhusiwa Sheikh Ponda kupanda jukwaani.
Sheikh Ponda mara baada ya kumaliza kuongea, watu wakaanza kutawanyika,
lkn ghafla mwendesha shughuli akatangaza waislam wasitawanyike kwanza
kwa kuwa kulikuwa na matangazo.Wakati matangazo yanendelea ambayo
sikuweza kuyasikia , ghafla tukaona defenda moja ya polisi inaingia
ambayo ilikuwa imejaza polisi walio tayari kwa mapambano. Waislam wakawa
wanawashanga kulikoni tena ilhali mkutano ulifanyika na kuisha kwa
amani kabisa.
Basi Sheikh Ponda akaingizwa kwenye taxi iliyokuja kumfuata akiambatana
na Sheikh Kondo Bonge. Polisi walitaka kumkamata sheikh Ponda lakini
waumini wakamkinga kwa kulizingira gari alilopanda sheikh Ponda huku
likiondoka taratibu. Huku nyuma gari la polisi likawa linafuata taratibu
bila kubiga risasi hewani wala kupiga mabomu ya machozi. Gari ya
polisi ilipofika barabara ya lami maeneo ya karibu na jengo la Fire
ilionekana kusima kwa muda huko gari iliyombeba sheikh Ponda kukunja
kushoto kueleke kwenye msikiti wa Mungu mmoja dini moja. Kabla msafara
wa Ponda haujafika kokote gari nne za polisi zilikuja kwa kasi sana na
kuanza kupiga mabomu ya machozi kuwatawanya waumini, watu walitawanyika
na Sheikh Ponda akashuka na kuelekea kwenye Gereji moja hivi kabla ya
kufika idara ya maji ambako ndiko alikopigwa risasi. Kwakweli sijui
ilikotoke risasi iliyompiga Ponda, nadhani kamanda wa polisi atalitolea
ufafanuzi zaidi. Mimi nimeandika kile nilichoona kwa macho yangu!
Mi nilidhani ingekuwa busara kwa jeshi la polisi kama walimuhitaji
sheikh ponda wangemwambia anahitajika polisi na hivyo ajisalimishe.
0 comments :
Post a Comment