Dar es Salaam. Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), imeyashtaki magazeti ya Mwananchi na The Citizen kwa madai ya kuchapisha habari zilizolenga kuichafua kampuni hiyo.
IPTL pamoja na Pan Africa Power Solutions Tanzania Limited na Harbinder Singh Sethi wamefungua kesi ya madai namba 47 ya mwaka 2014 katika Mahakama Kuu ya Tanzania wakitaka kuombwa radhi na kulipwa jumla ya Dola za Marekani 5.5 bilioni (Sh8.8 trilioni). Walalamikaji kupitia kampuni tatu za uwakili za Bulwark Associates Advocates, Mawalla Advocates na ASYLA Attorneys wanadai kuwa Machi 5, mwaka huu Gazeti la Mwananchi na mchapishaji wake Mwananchi Communications Limited (MCL) kwa pamoja walichapisha habari iliyolenga kuwakashifu mbele ya jamii.
Walalamikaji wamelishtaki pia Gazeti dada la The Citizen na mchapishaji wa magazeti hayo ambayo ni Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, kwa madai ya kuchapisha mfululizo wa habari zilizolenga kuichafua kampuni hiyo.
Katika mashtaka yake, wanadai gazeti hilo katika siku tofauti kuanzia Machi 3 hadi 12, mwaka huu ilichapisha mfululizo wa makala zilizokuwa na mwelekeo wa kuidhalilisha.
Kesi hiyo itatajwa kwa mara ya kwanza Juni 9, mwaka huu katika Mahakama Kuu ya Tanzania.
Kesi hiyo imefunguliwa wakati Serikali imeagiza suala hilo lichunguzwe na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa kushirikiana na Taasisi ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa (Takukuru
0 comments :
Post a Comment