
Kocha aliyetimuliwa hivi karibuni na klabu ya Manchester United David Moyes anachunguzwa na polisi wa Uingereza kutokana na tuhuma za kumsahmbulia kijana mwenye umri wa miaka 23 katika bar huko Lancashire, Uingereza. Inasemekana kuwa Moyes alikuwa anapata kinywaji kama walivyo wateja wengine lakini ghafla kukazuka mazungumzo ambayo yalimuhusisha kocha huyo wa zamani wa Everton na ndipo kukatokea shambulizi hilo lakini meneja wa bar amesema hakuna hasara yoyote aliyopata. Moyes anahusisha na kujiunga na klabu ya Celtic ya Scotland baada ya klabu hiyo kumtupia virago kocha wake Neil Lennon
0 comments :
Post a Comment