TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

Yerusalemu, Israel. Malumbano makali ya maneno na hoja yamezuka baina ya Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu kuhusu lugha gani aliyotumia Yesu Krtisto miaka 2,000 iliyopita.
Viongozi hao Jumatatu mchana wakati wa ziara ya siku tatu ya Papa aliyoifanya katika eneo la Mashariki ya Kati ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu atwae wadhifa huo. “Yesu aliishi hapa katika ardhi ya nchi hii. Alizungumzia Kiebrania,” alianza Netanyahu wakati akimweleza Papa Francis kwenye mkutano wa hadhara mjini Yerusalemu.
Netanyahu, pia akaeleza kuwa upo uhusiano wa karibu baina ya mahali alikozaliwa Yesu na Ukristo.
Naye Papa Francis akasikiliza kwa muda, kisha akajibu: “Yesu alizungumza lugha ya Kiaramaiki.”
“Ndiyo, nimesema alizungumza Kiaramaiki, lakini pia alijua Kiebrania,” akaingilia kati Netanyahu.

Chanzo Mwananchi

0 comments :

Top