Bunge la wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam wameipinga bajeti ya mwaka wa masomo wa 2014-2015 kiasi cha shilingi milioni 121 na hazina ya shilingi milioni 9.
Leo ilikuwa ni siku ya kikao cha bajeti ya serikali ya Wanafunzi wa chuo hicho chini ya DARUSO kilicho anza asubuhi kwa Waziri wa fedha kuwasilisha bajeti ya serikali ya DARUSO kwa mhula wa masomo 2014-2015.
Sababu ya kutoipitisha bajeti hiyo ni pamoja na Waziri wa fedha kuto onyesha mapato na matumizi ya magari yanayo iingizia pesa jumuia hiyo ya wanafunzi ya DARUSO, kitu kilicho washitua wabunge hao na kuona bajeti hiyo haijakamilika na hivyo inahitaji marekebisho makubwa kwani suara hilo ni nyeti saana
Sababu nyingine ni kutokana na utata wa juu ya suara la idadi ya viongozi wa DARUSO watakao baki kwa ajili ya kushughulikia wanafunzi watakao kuwa katika mafunzo kwa vitendo (field). kutokana na uzito wa jambo hilo katika kipindi chote cha serikali za nyuma, wamekuwa wakibaki viongozi watatu, lakini serikali ya mwaka huu chini ya Rais wa chuo FILBERT NIKSONI kwa kupitia Waziri wa fedha na uwekezaji, wakapendekeza kubaki kiongozi mmoja. Jambo ambalo liliibua mjadala wa hali ya juu sana ndani ya bunge hilo.
Suala lingine ni kuhusu kutelekezwa kwa wabunge katika jambo la fedha kwa ajili ya mawasiliano, kwani wabunge walipendekeza kuwa kila Mbunge apewe kiasi cha shilingi 250 kila sika kwa siku 240, kwa wabunge 118.
Mshauri wa Wanafunzi kila mara alionekana kunyosha mkono na kupewa nafasi ili asuruhishe jambo hilo lakini wabunge wakasimamia msimamo wao na ndipo Waziri wa fedha akakubali suala la kuwapa Wabunge shilingi 250 kila mtu kwa kila siku na kutotoa msimamo wowote juu ya idadi ya viongozi watakao baki kwa kila kitivo.
Spika wa bunge hilo la DARUSO alipo uliza kama wabunge wanaipitisha bajeti hiyo, na kama ilivyo desturi ya ndiyo au hapana, upande wa ndio yaani kuipitisha ukaonekana umeshinda kwa mujibu wa spika, lakini uamuzi huo ulipelekea malalamiko makubwa na Wabunge kuomba mwongozo kulingana na kanuni za bunge la DARUSO zinavyosema, kwa kuruhusu kura zihesabiwe iwapo mbunge yeyote hatoridhika na uamuzi huo
Wabunge wakapiga kura na wabunge wanaosema bejeti ipite wakapata kura 30 na wanaosema isipite wakapata kura 36 na hivyo kuamuliwa bejeti isipitishwe hadi hapo kutakapofanyiwa marekebisho hayo.
Hiki kilikuwa ni kikao cha pili cha bunge tukufu la Wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam, ambapo ndani ya bajeti hiyo, serikali ya wanafunzi wamepanga kununua TV flat screen 4 na kuunganisha na DSTV kwa ajili ya wanafunzi kupata habari kiulahisi zaidi.

0 comments :
Post a Comment