aadhi ya wakazi wa Dar es Salaam wanadaiwa kula samaki wanaovuliwa ndani ya mabwawa ya maji taka ya vyooni.
Uchunguzi uliofanywa, ulibaini kuwa samaki hao jamii ya kambare wanavuliwa kutoka kwenye mabwawa ya majitaka yanayomilikiwa na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam, (Dawasa), ni kitoweo cha wakazi waishio karibu na mabwawa hayo na wateja wengine.
Ulibaini zaidi kuwa uvuvi kwenye mabwawa hayo hufanywa na vijana wanaotumia nyavu za kuvulia samaki wanaoingia mabwawani nyakati za usiku.
Watu hao wanajitumbukiza kwenye mabwawa hayo yenye kinyesi bila kujali afya zao na kuvua kambare na perege wanaowauza mitaani kuanzia Sh. 300 hadi 2,000.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa baadhi ya watoto wenye umri kati ya miaka mitano hadi 16 wanavua samaki kwa kutumia vyandarua kisha huwachoma na kuwala wakiwa mabwawani.
BUGURUNI
Ziara ya Buguruni Kisiwani ilibaini kuwa kuna mabwawa matatu na eneo la Spenco Vingunguti nako kuna mabwawa kadhaa Katika eneo hili gazeti hili lilikutana na watoto waliokuwa wakivua kula samaki wa maji taka baada ya kuwabanika.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizo, walimueleza kuwa mara wanapopata samaki mkubwa wanamchoma na kufaidi kitoweo.
“Tunavua samaki wadogo wakati mwingine tunapata wakubwa zaidi ambao tunawala,” alisema mmoja wao mwenye miaka tisa jina linahifadhiwa kwa sababu ya umri.
Alisema zamani walipokuwa wakiishi karibu na mabwawa ya maji hayo huko Vingunguti Spenco aliona watu wazima wakiwavua na kuwauza.
Hata hivyo, watoto hao licha ya kutambua maji hayo ni machafu wanafanya hivyo kutokana na kuwaona watu wazima wakila kitoweo.
Andrew Ruta mkazi wa Buguruni Kisiwani ambaye anaishi karibu na mabwawa hayo, alisema miezi miwili iliyopita aliwaona vijana wakivua kwenye moja ya mabwawa hayo.
“Kati ya saa 5:00 au saa 6:00 usiku nilitoka nje na kuwakuta vijana wakiwa na nyavua wakivua samaki mabwawani hapo,”alisema Ruta.
Aliongeza kuwa, mara nyingi mchana watoto wanacheza sehemu hizo na wengine wanavua samaki licha ya kufukuzwa mara kadhaa na walinzi wa Dawasa.
“Wazazi wao ndiyo wazembe huwezi kumuacha mtoto achezee maji taka, tunapowaona humo tunawafukuza lakini wakitumuliwa wanarudi tena,” alisema.
Akilipoulizwa kuhusu milipuko ya magonjwa alisema maradhi yanapotokea wanatoa taarifa Dawasa ili wanyunyizie dawa za kuondoa harufu na kuua wadudu.
Mlinzi wa kampuni binafsi inayolinda mabwawa hayo, Amina Athuman, anayelinda mchana alisema mwaka jana alishuhudia vijana wakivua lakini aliwapa onyo.
“Sijawahi kuwaona mchana wakifanya hivyo, labla wanaogopa mwanga ila wanaotusumbua ni watoto wanaingia kuvua samaki wadogo kwa nyavu zao wanazotengeneza,” alisema.
Alibainisha kuwa vitendo hivyo vinafanyika kwa vile hakuna ulinzi na wakati mwingine mabwawa hayo yanalindwa na mlinzi mmoja mchana na usiku bila kujali a ukubwa wa eneo.
Pia alisema mabwawa hayo hayana vibanda vya kujikinga na mvua au jua hivyo mlinzi kulazimika kukaa kwenye nyumba za watu.
"Usiku hali huwa mbaya zaidi kwa sababu eneo hili linafunikwa na giza kwa hiyo ni rahisi watu kuingia na kuvua samaki bila kuonekana,” alisema.
Ofisa Mtendaji wa Serikali ya Mtaa wa Buguruni Kisiwani, Regina Foya, alisema kwenye mabwawa hayo kuna kambale na kwamba taarifa za uvuvi walizipokea mwaka jana na kuimarishwa ulinzi.
Alipoulizwa kuhusu uvuvi kuendelea eneo hilo alisema hana taarifa.
Mkazi wa bonde la Kigogo CCM jirani na Mto Msimbazi eneo yanakotiririka maji ya viwandani, Abraham akizungumzia uvuvi wa samaki mtoni hapo alisema, baadhi ya watoto wanavua samaki, lakini hana taarifa iwapo wanawala au kuwauza.
Ilishuhudia wanafunzi Shule ya Msingi Kigogo ambao mara baada ya masomo wanakimbilia kuvua samaki na kuwabanika na kuwala.
Alisema licha ya maji ya mto huo kuwa machafu kwa vile yamechanganyika na uchafu wa vyooni na maji taka ya viwandani watoto wanavua bila hofu.
“Ukikaa hapa kuanzia asubuhi mpaka jioni, utaona maji yanabadilika rangi mara yanakuwa ya kijani , baadaye mekundu, wakati mwingine myeusi, kwa kweli maji haya siyo salama kwa binadamu na viumbe wengine,” alisema.
Aliiomba mamlaka za usafi na mazingira kushughulikia uchafuzi wa mto huo unaofanywa na viwanda kwani maji yake yenye taka za sumu na kinyesi hutumiwa kumwagilia bustani za mboga.
“Dar es Salaam kila tunachokula naona siyo salama, ukisema usile samaki ule mboga za majani, uzalishaji wake unatumia maji machafu,” alisema na kushauri mamlaka hizo zitoe elimu ya utunzaji wa mazingira na kutumia maji safi kwenye kilimo.
Via Nipashe Jumapili. Picha na Vitendo

0 comments :
Post a Comment