| Picha za hivi karibuni za Vera Sidika kwenye mitandao ya kijamii |
Swala la kubadili rangi ya ngozi limekuwa kama msumari moto,
kunao wanaoliunga mkono na wale wanaolipinga swala hilo katu hawawezi
kulifanya.
Baadhi wanasema kuwa ni wanawake wasiojithamini na kujiamini pekee ndio wenye
kujichubua ngozi.
Mjadala huo ukiendelea, wasichana wengi wanajitafutia umaarufu sio Marekani
na Uingereza tu bali hata katika kanda ya Afrika ya Mashariki. Wasichana hao
wamekuwa wakifanya kila wawezalo ili kupata huo umaarufu.
Mmoja wa wasichana hao ni Vera Sidika anayejulikana sana nchini Kenya na
Afrika mashariki kwa kuwa na makalio makubwa ambayo ndiyo yaliyompa umaarufu
wake baada ya kuonekana katika wimbo mmoja wa video uitwao 'You Guy' ambao
baadaye ulipigwa marufuku nchini Kenya.
Picha za awali kabla ya Vera kujichubua ngozi
Vera amejizidishia umaarufu kwa kubadili rangi yake ya ngozi, zamani kidogo
akiwa mweusi na sasa amejichubua na kuwa mweupe na pia kuwaambia watu kuwa
kubadili rangi ya ngozi yake ni yeye mwenyewe kujitakia. Hiyo isiwashughulishe
watu.
Vera anajulikana kwa kuwa na mazoea ya kujipiga picha hasa za makalio yake na
kuziweka kwenye mitandao ya kijamii. Vara analinganishwa sana na Kim Kardhashian
hasa kwa sababu ya umbo lake.
Kazi ya Vera hasa ni ya uwanamitido lakini mbali na hilo Vera hulipwa ili
kufika kwenye karamu mbali mbali , kwenye disco na katika hafla mbali mbali za
watu mashuhuri. Yeye pia hulipwa kuwa katika kanda za video za wanamuziki
maarufu Afrika Mashariki.
Alifichua kupitia televisheni Ijumaa kuwa alitumia maelfu ya dola kubadili
rangi ya ngozi yake na kujifanya mweupe.
Shughuli hiyo aliifanyia nchini Uingereza na ilimgharimu karibu milioni 15
pesa za Kenya, hizo ni dola 170,000 na kwamba tayari kuna watu wengi wanaotaka
sana kujichubua ngozi na kufanana na Vera, kwa mujibu wa mwanadada huyo.
Vera ni mwanamitindo na anapanga kufungua duka la kuuzwa bidhaa
za urembo
Vera anasema kuwa watu wamemsema sana kwenye mitandao ya kijamii vibaya kwa
sababu ya anavyoendesha maisha yake. Amewataja kama wanafiki kwa sababu anasema
huku wakiendelea kumsema na kumkosoa kwa kujichubua, wamekuwa wakimuuliza
alichofanya ili na wao watafute pesa wakafanye hivyo kwa wanataka sana kufanan
naye.
Mtindo wa wanawake kujichubua ni swala tata nchini Kenya. Sio kama India
ambako vipodozi vya kujichubua huuzwa wazi wazi. Nchini Kenya bidhaa hizo,
huuzwa kimagendo.
Wataalamu wanasema, wanawake wengi wanaendelea kujichubua licha ya hatari za
bidhaa zinazouzwa kimagendo.
Swala la wanawake kijichubua barani Afrika lilianza kujadiliwa waziwazi pale
ambapo msanii raia wa Cameroon Dencia kuzindua rasmi bidhaa zake za kuchubua
ngozi ziitwazo, Whitenicious.
Chanzo BBC
0 comments :
Post a Comment