Wanafunzi wa vyuo vikuu wanakusudia kufanya mgomo nchi nzima, kulishinikiza Jeshi la Polisi kuelekeza alipo Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanafunzi ya Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO), Musa Mdede.
Mdede ambaye pia ni Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Sayansi ya Afya na Tiba cha Bugando (KUHASA) mkoani Mwanza , Musa Mdede, anadaiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha katika tukio linalosadikiwa kuwa ni la utekaji nyara jumatano iliyopita.
Mdede alidaiwa kupotea mda mfupi akiwa akijiandaa kwenda kurudisha fomu ya kuomba kutetea nafasi yake katika uchaguzi wa viongozi wa setikalihiyo.
waziri mkuu wa serikali ya Wanafunzi hao, Benjamimni Thomas, alithibitisha Mdede kukumbwa na masaibu hayo na kusema hawakuwa na taarifa zozote kuhusu kuhusu kupotea kwake
0 comments :
Post a Comment