TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749



Dar es Salaam. Dar es Salaam. Kocha mkuu wa Azam FC, Joseph Omog amewasilisha maombi matatu kwa uongozi wa timu hiyo yanayotakiwa kufanywa kwa haraka huku akisema hataki kambi ya nje ya nchi.
Akizungumza na gazeti hili, Mwenyekiti wa Azam FC, Said Mohamed alisema wamepokea ripoti ya Omog ambayo kwanza ameupongeza uongozi wa timu hiyo kwa kumsajilia timu ya nguvu itakayoweza kutetea taji la ubingwa wao, lakini akawashangaza viongozi wake kwa kusema hataki kambi ya nje ya nchi kwa kuwa Chamazi Complex panatosha.
Said alisema mbali na Mcameroon huyo kugomea kambi hiyo pia ameutaka uongozi wake kumtafutia mechi nyingi za kirafiki kila wiki bila kujali aina ya timu.
Alisema mbali na hilo Omog amewaomba uongozi wake kusaka kiungo mshambuliaji wa pembeni kutoka ndani ya nchi ambapo kazi hiyo bado inaendelea kufuatia kocha huyo kubaini upungufu katika eneo hilo.
“Tumepokea ripoti ya kocha wetu mwishoni mwa wiki iliyopita ametuagiza tumtafutie mechi za kirafiki sasa nimeshawaagiza watu kuanza kazi ya kutafuta hizo mechi haraka,” alisema Said.
“Ukiacha hilo kocha wetu amekataa katakata kuiondoa timu hapa nchini kwa lengo la kuweka kambi kama tulivyokuwa tukifanya huko nyuma, tulimuuliza endapo atahitaji kambi ya nje akatuhoji ya nini wakati huko kuna mazingira tofauti na haya ya hapa ambako ligi inachezwa, lakini zuri zaidi ametuambia Chamazi kuna kila kitu anachohitaji nasi tumemkubalia.
Aliongeza: “pia anataka tumtafutie kiungo mmoja wa pembeni kutoka hapa hapa nchini na ndio tunahangaika kuhakikisha tunapata mchezaji huyo kwani hatutaki kumuuzi kocha kwani yeye ndiye anayejua mapungufu ya timu yake.”
Azam mwaka jana iliweka nchini Afrika Kusini kujiandaa na Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho wakati huo ikinolewa na kocha Muingereza, Stewart Hall, lakini hata hivyo kocha huyo aliifundisha timu hiyo mzunguko wa kwanza tu kabla ya kumuachia Omog aliyeipa ubingwa wa kwanza wa Ligi Kuu klabu hiyo.
Subhead andika hapa , andika hapa,andika hapa Subhead andika hapa andika, andika hapa, subhead andika hapa, andika hapa,

0 comments :

 
Top