![]() |
Leo kulikuwa na mdahalo wa katiba mpya ulioandaliwa na UDASA toka chuo kikuu cha Dar es salaam, na kongamano hilo lilifanyika katika ukumbi wa Nkuruma chuo kikuu cha Dar es salaam huku ukiongozwa na Dr Wilbroad Slaa(mwakilishi wa UKAWA), Mh Steaven Wasira (mwakilishi wa CCM), Dr Kitila Mkumbo na Prof Gaudensi Mpangala.
Katika kongamano hilo lililokuwa limeandaliwa kwa lengo la kutafuta muafaka wa kuja ni naani anaye kwamisha upatikanaji wa katiba mpya, kulikuwa na hoja nzitozilizo kuwa zikitetea kwa nini ukawa wametoka nje ya katiba na kwa nini wanahitajika kurudi ndani ya Bunge, ili kuendelea kujadili na kutengeneza katiba mpya.
Jambo ambalo lilikuwa la kipekee katika Kongamano hilo, ilikuwa ni kutawaliwa na vijana wenye umri mdogo wengi saana, jambo ambalo lilikuwa likiibua shangwe nyingi saana pindi Waisra anapo wasilisha hoja zake na kuzomea pale Lisu alipokuwa anajaribu naye kuwasilisha hoja zake. Kitendo hiki kilichukuliwa kama ukomavu kwa vijana, lakini kumbbe ilikuwa sio.
Idadi kubwa ya vijana waliokuwa wamejitokeza katika kongamano hilo, k,umbe walikuwa wamesombwa na viongozi wa CCM toka maeneo mbalimbali kama vili, Tabata, Magomeni, Gongo la mboto, Ubungo na maeneo mengine.
Vijana hao pamoja na kina mama na wazee wachache, walikuwa wameletwa katika kongamano hilo kwa kutumia usafiri wa UDA, ambapo kulikuwa na magari matano yaliyo kuwa yamesheheni makada wa CCM kutoka maeneo mbalimbali.
Katioka ukumbi huo, asilimia kubwa ya viti vyoote ikiwa ni pamoja na vile vya VIP, vilikuwa vimejazwa na umati wa watu hao walioletwa na viongozi wao wa CCM, huku wanfunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam walio hudhulia katika mdahalo huo wakiwa kama mashahidi tu wa mjadala huo kwani hata siti tu hawakupata.
Tulipo fanya mahojiano na baadhi ya vijana, walikubali kuwa wameletwa na viongozi wao wa CCM na kazi yao kubwa waliyoambiwa ni kuzomea pale mtu anapotetea serikali 3 na kushangilia mtu anayetetea serikali 2, huku wakiwa hawana uelewa wa kutosha juu ya mchakato wa katiba wenyewe.
Pia walieleza kuwa wamepewa baadhi ya malipo ikiwa kama kifuta jasho kwao, kama vile pesa ya maji, chakula na kikinga mfuko. Huku wale wa kutoka Kinondoni wakiwa wameahidiwa chakula baada ya kongamano kuisha.
Baadhi ya majina ya viongozi wa CCM walio husika katika kuwakusanya vijana hao ni pamoja na Fikili Magoso katibu wa CCM Kinondoni na na Peter Joakim, kutoka Tabata.
Kitu cha kushangaza zaidi ni pale kiongozi mmoja toka CCM alipotishia kumfukuzisha chuo mwandishi wetu kwa kosa la kuchukua namba za magari yaliyotumika kubeba watu hao.
Msimamo wa UKAWA
Ukawa bado wameendelea kuwa na msimamo wao wa kuto taka kurudi bungeni kwani wanaamini kuwa hata wakirudi bado CCM wanaweza kuendelea na ubnabe wao wa kutaka mambo yao ndiyo yapitishwe. haya yalionekana pale Tundu Lisu alipo kuwa akijibu swali toka kwa Dr Mkumbo, lililokuwa linataka UKAWA waeleze ni kwanini hawataki kurudi bungeni ingawa kunasuti nyingi saana zinazo washauri kurudi bungeni ili waendele na mjadala wa katiba mpya.
Lisu alisema kuwa kutokana na mabadiliko ya kanuni za bunge zilizofanywa na wabunge wa CCM baada ya UKAWA kutoka bungeni, inaonyesha zahiri kabisa kuwa katiba itatungwa kutokana na mapendekezo ya chama chao na hivyo bado maamuzi ya wananchi yanaweza yasichukuliwe na kuchakachuliwa pia, kitu ambacho kinaweza kulipeleka taifa mahala pabaya.
"Hii inaweza kufanyika kama ilivyofanyika Kenya baada ya kudharauliwa mapendekezo ya wananchi, ikapelekea machafuko makubwa na mpaka sasa, Rais wa Kenya anakesi katika mahakama ya kimataifa"
Kwa upande wa Wasira alipoulizwa kwanini CCM haikubali mfumo wa serikali tatu na kuachana na msimamo wa mbili kwa kuwa nfumo wa serikali 3 umeanza kupendekezwa na makada wa CCM waliobobea wenyewe, kama vile, Nyalali, Warioba, na wengine
Wasira alisema kuwa CCM ni taasisi na hivyo haiwezi kuchukua mawazo ya mtu mmoja mabaye ameleta matokea na mapendekezo ambayo hakuambiwa alete, hayawezi kukubaliwa.
![]() |
| Mtoto huyu naye alikuwemo katika walioletwa huku akiwa hajui alichokuja kufanya zaidi ya kupiga makofi na kuzomea |
![]() |
| Gari likiwa limewabeba watu toka CCM tayari kwa safari ya kurudi makwao na UDA |
![]() |
| Baadhi ya vijana waliokuwa wameletwa na CCM |
![]() |
| Watu wakiwa wanafuatilia mjadala |
![]() |
| baadhi ya wananchi wakifuatilia kongamano hilo |






0 comments :
Post a Comment