TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

Mjumbe wa Bunge la Katiba, John Cheyo (UDP) amesema hakuna mantiki ya watu kuwazungumzia wajumbe waliosusia vikao.
Akizungumza mjini Dodoma, Cheyo alisema kuwa vikao vimeanza lakini hakuna sababu ya kuwabeza wale ambao wamekataa kurejea bungeni.
Akichangia mjadala wa kanuni katika kikao cha juzi, Cheyo alisema si busara kubeza uamuzi wa waliokataa kurejea katika Bunge hilo kwa kuwa ni watu wazima wenye akili tumamu na wana sababu za kufanya hivyo, kwa hiyo kuanza kuwakejeli ni suala lisilokuwa na tija kwa taifa.
Aliwaeleza wajumbe wa Bunge hilo kwamba wanatakiwa kujua kwa nini wao wameamua kurejea na kuendelea na Bunge hilo na kwamba Watanzania wana uwezo mkubwa wa kuchambua na kuwasoma na kisha kuchambua mbivu na mbichi.
“Nawaomba tusitumie muda mwingi kuwabeza wale ambao hawapo hapa. Wale ni watu wazima na wanajua kwamba kwa nini hawapo hapa.
Kuna mambo mengi sana yanayotukabili na tunahitaji kuyajadili na kuyapatia ufumbuzi kwa sasa. Hiyo ndiyo kazi yetu,” alisema Cheyo.
Alishauri kwamba hakuna haja ya kuharakisha kupata Katiba mpya kwa sababu tu tunaelekea katika uchaguzi mkuu wa mwakani, na ikibidi inaweza kufikia hatua hata mchakato huo ukaahirishwa ili kupata Katiba mpya yenye masilahi kwa Watanzania na si ya kuipeleka nchi katika uchaguzi.
Alisisitiza kwamba Katiba mpya ni zaidi ya kuamuliwa tu kwa wingi wa waliomo bungeni, kwa kuwa inahitaji kupata maridhiano baina ya walio wengi na walio wachache, ili dhana ya kuwa na katiba ya Watanzania iweze kukamilika.
Source Mwananchi

0 comments :

 
Top