TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

Mjumbe wa Bunge la Katiba, Ezekiah Oluoch ametaka kuahirishwa kwa vikao vya chombo hicho na mabilioni ya fedha yatakayookolewa yaelekezwe katika malipo ya walimu ambao wanadai malimbikizo yao serikalini.
Akizungumzia umuhimu wa kutoendelea kwa Bunge hilo lililoanza juzi, Oluoch alisema si busara kuendelea kutumia mabilioni ya fedha za walipa kodi kwa kuendelea na vikao vya chombo hicho cha kuandika katiba kwa kuwa matokeo yake huenda yasiwe na manufaa kwa Watanzania.
“Ninavyozungumza hapa kuna zaidi ya walimu 38,000 hawajalipwa madai yao kwa maelezo kwamba Serikali haina fedha.
“Lakini hapa kwa wiki moja tayari wabunge wamelipwa Sh2 bilioni. Afadhali bunge hili liahirishwe na kuokoa Sh18 bilioni, halafu zielekezwe kulipa madeni ya walimu,” alisema Oluoch.
Kauli hiyo ilizua kelele miongoni mwa wabunge, na wengi walionekana kucheka na wengine wakieleza kuwa ni lazima Bunge hilo liendelee kama ilivyopangwa na lazima walipwe posho.
Source Mwananchi

0 comments :

 
Top