TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749



Wasanii wengi sana hutunga nyimbo kwa kuandika mistari ambayo wanaona itaendana na mapenzi ya mashabikiwake. Hali hii hufanya watunge ujumbe ambao huwa unailenga jamii moja kwa moja na kuchukua ujumbe huo kama wameandikiwa wao kwa kuwa wanakuwa wanaguswa.

Lakini kunawengine huwa wanatunga nyimbo kulingana na uzoefu walionao katika maisha yao na simulizi za mikasa yabaadhi ya rafiki zao.

Lakini hii imekuwa tofauti kwa msanii Christian Bella ambaye amesema alitunga wimbo wake wa 'Nani kama mama' baada ya kumshuhudia live mke wake akijifungua na kupata mateso makali, hivyo aka-salute kuwa mwanamke anatakiwa kuheshimiwa tofauti na anavyochukuliwa.
Kama nawe unaamini mama yako anastahili heshima kubwa, comment neno 'Asante mama'

0 comments :

 
Top