TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

                     


Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam, linamshikilia na kumhoji mtu mmoja aitwaye Robson Seif Emmanuel, mwenye umri wa miaka 30 mkazi wa Kijitonyama jijini Dar es salaam, kwa tuhuma za kujifanya afisa wa Polisi kikosoi cha usalama barabarani, huku akiwa anafanya kazi ya kukagua makosa ya usalama barabarani.
 Mtuhumiwa huyo alikamatwa tarehe 02/08/2014 katika Kata ya Chamazi, Mbagala Majimatitu Temeke akiwa amevaa sare ya za polisi na cheo cha Stesheni Sajenti.
Mtuhumiwa alikutwa na gari aina ya Cresta lenye namba ya usajili T723 BAK, analolitumia kuzungukia maeneo mbali  mbali ya jiji akiwadanganya watu kuwa yeye ni askari polisi
Ndani ya hilo gari kulikutwa na
-Radio call 1 yenye namba GP380 aina ya Motorola
-Leseni za udereva 40, za watu mbalimbali
-Polis Loss Report mbalimbali
-Nakala 3 za notification  zilizo jazwa
-Kofia moja ya (Uhuru Cape) ya usalama barabarani
-Beji 1 yenye jina la E.R. MWAKYUSA ya kuweka kifuani
-Ratiba ya mabasi yaendayo mikoani ya SUMATRA

Pia mtuhumiwa alifanyiwa ukaguzi nyumbani kwake na kukutwa na vitu vingi saana kama vile
-Pea 4 za sare ya Polisi ya kaki
-Pea 3 za sare ya Polisi ya Usalama barabarani
-Koti 1 la mvua la Usalama barabarani
-Refrector 8 za Usalama barabarani
-Kofia 1 (Uhuru Cape) ya Usalama barabarani
-KOfia  2 (Barret) nyeusi za Polisi
-Mikanada miwili ya Bendera mali ya Jeshi la Polisi
-Mikanda 2 ya Polisi (Tunic Cross Belt) mweusi
-Mikanda 2 ya filimbi
-Choe kimoja cha Sajenti
-Vyeo vi 4 vya Stesheni Sajenti
-Vifungi 8 vya chuma mali ya Jeshi la Polisi
-Cheo kimoja cha Stesheni Sajenti cha JWTZ
-Notification form zilizo jazwa  zipatazo 62
-PF3 forms zipatazo 4
-Notification forms ambazo hazijajazwa zipatazo 8
Baada ya uchunguzi kufanyika imegundulika kuwa mtuhumiwa aliwahi kuwa askari polisi, aliyejiunga na Jeshi hilo Mwaka 2000, akiwa mwenye namba F2460, lakini alifukuzwa kazi kwa fedheha mnamo tarehe 21/03/2014, huko Kibaha Mkoani Pwani akiwa na cheo cha Stesheni Sajenti.
Mtuhumiwa amekuwa akijitambulisha kama yeye ni askari hivyo kufanikiwa kutapeli wananchi mbalimbali na kujipatia kiasi kikubwa chafedha.
Wananchi waliotapeliwa wanaombwa kufika polisi ili kuchukua mali zao na sheria ichukue mkondo wake kwa mtuhumiwa.

0 comments :

 
Top