Kwa upande wa viongozi wa kisiasa ambao waliingiziwa fedha katika akaunti zao binafsi ni; Mhe. Andrew Chenge (Mb), ambaye alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na sasa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, shilingi bilioni 1.6; Mhe. Anna Tibaijuka (Mb) na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi shilingi bilioni 1.6; Mhe. William Ngeleja (Mb) na ambaye alikuwa Waziri wa Nishati na Madini shilingi milioni 40.4 na Ndg. Daniel N. Yona ambaye alikuwa pia Waziri wa Nishati na Madini shilingi milioni 40.4; Ndg. Paul Kimiti ambaye ni Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Sumbawanga shilingi milioni 40.4 na Dr. Enos S. Bukuku ambaye alikuwa Mjumbe wa Bodi ya TANESCO aliingiziwa shilingi milioni 161.7.
Upande wa Viongozi wa Madhehebu ya Dini walioingiziwa fedha na Benki ya Mkombozi ni Askofu Methodius Kilaini shilingi 80.9, Askofu Eusebius Nzigirwa shilingi milioni 40.4 na Mchungaji Alphonce Twimann Ye Simon shilingi milioni 40.4
Kamati ilithibitishiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU kuwa baadhi ya watu walienda kugawana fedha kwenye Benki tajwa wakiwa na mifuko ya rambo, sandarusi, mabox, magunia na lumbesa. Kutokana na muamala uliofanyika tarehe 6 Februari, 2014 katika Benki ya Mkombozi kiasi cha shilingi bilioni 3.3 na muamala wa Benki ya Stanbic wa tarehe 23 Januari 2014 ambapo fedha taslimu (cash) kiasi cha shilingi bilioni 73.5 zilitolewa na kugawanywa kwa watu mbalimbali kinyume cha Sheria ya Benki Kuu na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006
Upande wa Viongozi wa Madhehebu ya Dini walioingiziwa fedha na Benki ya Mkombozi ni Askofu Methodius Kilaini shilingi 80.9, Askofu Eusebius Nzigirwa shilingi milioni 40.4 na Mchungaji Alphonce Twimann Ye Simon shilingi milioni 40.4
Kamati ilithibitishiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU kuwa baadhi ya watu walienda kugawana fedha kwenye Benki tajwa wakiwa na mifuko ya rambo, sandarusi, mabox, magunia na lumbesa. Kutokana na muamala uliofanyika tarehe 6 Februari, 2014 katika Benki ya Mkombozi kiasi cha shilingi bilioni 3.3 na muamala wa Benki ya Stanbic wa tarehe 23 Januari 2014 ambapo fedha taslimu (cash) kiasi cha shilingi bilioni 73.5 zilitolewa na kugawanywa kwa watu mbalimbali kinyume cha Sheria ya Benki Kuu na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006
Aidha Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na
Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) mara moja wachukue hatua ya
kumkamata Bwana Harbinder Singh Sethi na kumfikisha mahakamani kwa
makosa ya Anti money laundering , ukwepaji kodi na wizi. Kamati pia
inaelekeza Serikali kutumia sheria za Nchi, ikiwemo sheria ya ‘ Proceeds
of Crime Act ’ kuhakikisha kuwa Bwana Harbinder Singh Sethi anarejesha
fedha zote alizochota kutoka Benki Kuu ya Tanzania. Kwa kuwa suala hili
ni suala la utakatishaji wa fedha haramu, Mamlaka ziwasiliane na mamlaka
za Nchi nyingine kuhakikisha mali za Bwana huyu zinakamatwa na kufidia
fedha hizo.
Kwa mujibu wa Taarifa ya CAG na kuthibitishwa na Mkurugenzi Mkuu wa
TAKUKURU fedha hizo pia ziligawiwa kwa watu mbalimbali binafsi. Kamati
haina tatizo na watu wawili kuuziana makampuni yao kwa thamani wajuazo
wenyewe, au jinsi ya kuzitumia fedha zao, ama kuwachagulia watu wa
kuwagawia, lakini Kamati imejidhihirishia kuwa fedha iliyotumika kulipia
manunuzi hayo ni fedha ambayo sehemu yake ni ya umma iliyochotwa bila
huruma wala aibu, kutoka Benki Kuu. Hivyo, Kamati inazitaka mamlaka za
uchunguzi kuhakikisha kuwa fedha hizo zinarudi Benki Kuu hata ikibidi
kwa kufilisi mali za watu wote 97 waliofaidika na fedha hizo kwa thamani
ya fedha walizopewa na Bwana Rugemalira
Baadhi ya waliofaidika na fedha hizo ni Viongozi wa Umma ambao wanapaswa
kuzingatia Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma (Sheria namba 13 ya
Mwaka 1995) ambayo inawataka kutoa taarifa ya zawadi wanazopokea au
malipo wanayolipwa. Vyombo vya uchunguzi vifanye uchunguzi kutambua kama
walifuata matakwa ya sheria na hatua mahsusi zichukuliwe, ikiwemo
kuvuliwa nyadhifa zao zote za kuchaguliwa na/au kuteuliwa, kufilisiwa
mali zao na kushtakiwa mahakamani kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, ibara ya 132 (1) – (6).
Kamati imejiridhisha kwamba, suala la akaunti ya Escrow ni jambo la
utakatishaji wa fedha (Money Laundering), kama alivyosema Mkurugenzi
Mkuu wa TAKUKURU katika mahojiano yake na Kamati. Kamati inazitaka
mamlaka zinazohusika, ikiwemo Benki Kuu kuzitangaza benki za Stanbic na
Mkombozi Commercial Bank kama asasi za utakatishaji fedha (Institutions
of Money Laundering Concern).
Aidha, Kamati inalikumbusha Bunge lako tukufu pendekezo
muhimu lililotolewa na Kamati Teule ya Mheshimiwa Dkt. Harrison
Mwakyembe kuhusu sakata la maarufu la Richmond
Kamati inapendekeza kwamba, azimio hili litekelezwe kwa kupitia upya mikataba yote ya umeme ambayo inalitafuna Taifa letu.
Aidha, Kamati imebaini kuwa Waziri wa Nishati na Madini ndiye alikuwa
dalali mkuu aliyewakutanisha Bwana Harbinder Singh Sethi na Bwana James
Rugemalira, tena katika ofisi ya Umma; na pengine hii ndiyo iliyokuwa
sababu ya upotoshaji huu. Waziri wa Nishati na Madini alifanya udalali
huo akijua dhahiri kuwa Bwana Sethi hana uhalali wa kisheria kufanya
biashara kwa jina la IPTL. Iwapo Waziri wa Nishati na Madini angetimiza
wajibu wake ipasavyo, Fedha za Tegeta ESCROW zisingelipwa kwa watu
wasiohusika, na Nchi ingeweza kuokoa mabilioni yaliyopotea kama kodi za
VAT, Capital Gain Tax na Ushuru wa Stempu ambazo ni sawa na takribani
shilingi bilioni 30.
Mheshimiwa Spika, Kamati inapendekeza kuwa Mamlaka yake ya uteuzi
itengue uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini kutokana sababu hizo
zilizoelezwa.
Kamati pia imethibitisha uzembe wa hali ya juu uliofanywa na Katibu Mkuu
huyo, kushindwa kujiridhisha kama masharti ya Sheria ya kodi ya Mapato
Sura ya 333, Kifungu cha 90(2) yalitekelezwa. Kifungu hicho kimsingi
kinaitaka mamlaka ya ‘ approval ’’ ya uhamishaji wa Makampuni kutotambua
Kampuni mpaka kwanza kodi za uhamishaji ziwe zimelipwa na hati za
malipo ya kodi zimetolewa na mamlaka ya kodi. Mheshimiwa Spika, Kamati
inapendekeza kuwa uteuzi wa Katibu Mkuu huyu utenguliwe, na TAKUKURU
wamfikishe mahakamani mara moja, kwa kuikosesha Serikali Mapato,
matumizi mabaya ya ofisi na kusaidia utakatishaji wa fedha haramu.
Kamati imethibitisha kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali alitoa ushauri
ulioipotosha Benki Kuu ya Tanzania kuhusiana na hukumu ya Jaji Utamwa J.
Kwa kutumia madaraka yake vibaya, Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliagiza
kodi ya Serikali yenye thamani ya shilingi 21 bilioni isilipwe 106 na
hivyo kuikosesha Serikali mapato adhimu. Mwanasheria Mkuu wa Serikali
kwa kujua na kwa makusudi alilipotosha Bunge na Taifa kwamba mgogoro
uliopelekea kufunguliwa kwa Akaunti ya ESCROW ulikuwa ni mgogoro wa
Wanahisa wa IPTL badala ya mgogoro kati ya TANESCO na IPTL. Kamati
inapendekeza kuwa uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali utenguliwe mara
moja na kisha afikishwe mahakamani kwa matumizi mabaya ya Ofisi
yaliyopelekea Serikali kupoteza mabilioni ya fedha.
Baada ya kupitia vielelezo vilivyomo kwenye ripoti ya
CAG, Kamati imejiridhisha pasipo mashaka kuwa, Waziri Mkuu, alikuwa ana
taarifa zote kuhusiana na mchakato mzima wa kuchotwa fedha kutoka katika
akaunti ya ESCROW.
Kamati, kwa kuzingatia kielelezo namba 22, inathibitisha
bila shaka kwamba, Waziri Mkuu alikuwa analijua jambo hili vizuri na
kwamba aliridhia muamala huu ufanyike. Ndiyo maana katika maelezo yake
ya Bungeni mara kadhaa Waziri Mkuu alithibitisha kuwa fedha za Escrow
hazikuwa fedha za Umma.
Ni dhahiri kwamba viongozi wenye mamlaka makubwa
wanapaswa kila wakati kukumbuka kauli ya muasisi wa Mapinduzi ya
Zanzibar na Muasisi wa Muungano, Sheikh Thabit Kombo, ambaye alikuwa
akipenda kusema ‘ weka akiba ya maneno.
Kwa uzito na unyeti wa jambo hili, kwa vyovyote vile, Waziri Mkuu
anapaswa kuwajibika kwa kauli zake na kwa kutokutekeleza wajibu wake wa
kikatiba ipasavyo, ili kurejesha imani ya wananchi kwa serikali yao na
viongozi wao wa kisiasa.
0 comments :
Post a Comment