Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya UYUI mkoani TABORA
imethibitisha tukio la ajabu la kuinuka kwa mti aina ya MKALYA
ulioanguka kwa upepo mkali zaidi ya miaka mitano iliyopita na kuwataka
Wananchi wa kijiji CHESA kuulinda mti huo.
Mti huo unakuwa ni mti wa pili kuinuka wenyewe ndani kipindi cha
mwezi mmoja katika Kata ya UFULUMA wilayani UYUI, baada ya mti aina ya
MSUFI uliokuwa umeanguka na kulala chini kwa zaidi ya miaka mitatu
kuinuka wenyewe Oktoba Kumi na Tano mwaka huu.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya
TABORA{UYUI} ANSELIN TENDWA na Afisa Utamaduni wa wilaya hiyo DAUD
DANGUCHE wamesema watawasiliana na Watafiti ili waende kuutafiti mti
huo.
Wananchi wa kijiji hicho wamesema mti huo unatumika kwa tiba ya
asili na wameiomba Serikali iwajengee uzio kuzunguka eneo hilo kwa ajili
ya maonyesho
0 comments :
Post a Comment