Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amejisalimisha polisi kuhojiwa juu ya lugha aliyoitumia dhidi Polycarp Pengo.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam jana lilimtaka Gwajima afike Polisi, kwa sababu Kuna baadhi ya Sauti za kurekodiwa na video mitandaoni zinahusishwa naye zikimkashifu Askofu pengo.
Pamoja na kwamba leo kipande cha sauti kusambaa kuwa Gwajima angejisalimisha Jumatatu kwa kuwa kwa sasa yupo Arusha na kuwataka waumini wake kufika polisi Jumatatu bila kufanya vurugu. Kwa sababu ambazo hazijatolewa bado,
Askofu Gwajima amejisalimisha kituo cha Polisi tayari leo Ijumaa ili kuhojiwa juu ya kutoa lugha chafu dhidi ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo.
0 comments :
Post a Comment