TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

Mahusiano yana nafasi kubwa Katika maisha yetu ya kila siku, kwasababu kila mtu anahitaji upendo.
Ni njia zipi sahihi katika kuonesha upendo kwa tuwapendao ili kufanya mahusiano yaweze kudumu na kumfanya yule umpendaye ama anayekupenda kujua upendo wake kwako ama kwake.

Njia hizi kumi ni kati ya nyingi zinazosaidia mahusiano kukua na kudumu kwa muda mrefu;
1;sikiliza  (listen)
    Mahusiano yanahitaji kusikilizana na kuelewana. Sikiliza kwa maana ya katika kuonyesha upendo kwa uwapendao au umpendaye ni vyema kusikiliza nini anataka au nini wanataka au nini hawataki ama kutopenda.Pia mahusiano yenu mmoja wapo asipende kuwa yeye ndo muongeaji pekee bali pia kumpa mwenza wako nafasi kumsikiliza nini anasema.

2; Ongea (speak)
     Ongea kwa maana ya kuwa kueleza hisia zako ili umpendaye ajue vile unavyojisikia.

3;Toa (give)
    Onyesha upendo wako kwa yule umpendaye ili ajue. Na kutoa huko ni kwa vitendo na si maneno kwa mfano kujali, kumpa muda wako wa kukaa pamoja na kuongea mambo mbalimbali.

4;Sala au sali (pray)
   Katika mahusiano pia ni vema kumshirikisha Mungu ili kuweza kupita katika njia zake sahihi. Na  pia kwa kuwa yeye ndiye Muumba wa kila kitu hivyo sala ni muhimu na kumwomba yeye mahusiano yenu yapate kibali mbele zake.

5; Jibu (answer)
    Mahusiano pia yanahitaji mawasiliano ambayo ni sahihi, katika maongezi ni vema pia kila mtu awe anajaribu kujibu ama kufanya maongezi yawe ni ya baina yenu wote wawili. Na ili maelewano yawepo kumjibu mwenza wako ni muhimu. Angalizo -jibu ni kwa maana ya kwa suala au swali fulani ambalo lahitaji ufumbuzi baina ya wenza na si mabishano.

6; Shirikisha (share)
    Mahusiano yanahitaji kushirikishana baina ya watu ambao wako katika mahusiano.  Mfano katika kufanya maamuzi ni vema kila mmoja akamshirikisha mwenza wake.

7; Furahia au burudika (enjoy).
   Mahusiano yanahitaji kila mmoja afurahie mahusiano, hakikisha unafurahia mahusiano yenu na pia jitahidi kumfanya mwenza wako mwenye furaha.

8; Amini (trust)
   Uaminifu ni nguzo muhimu katika mahusiano, ni vema kujitaidi kuaminiana na kutokuweka hisia za kutokuaminiana.Kufanya vitendo kama kutokupokea simu,kuonana na mawasiliano hafifu.

9; Samehe (forgive)
    Mahusiano pia kuna kukoseana na hivyo ni vizur kuombana msamaha. Iwapo mmoja amekosea kujishusha ni muhimu ili kusaidia kudumu kwa mahusiano hayo.

10; Ahadi (promise)
    Mahusiano yana ahadi, iwapo mtu anatoa ahadi ni lazima atimize.kwasababu ahadi zisipotimizwa zinapelekea mahusiano kuyumba.Ni bora mtu usitoe ahadi kama unajua huwezi kutimiza.

    
   

0 comments :

 
Top