TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749



Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amehukumiwa kwenda jela mwaka mmoja au kulipa faini ya Shilingi milioni moja baada ya kupatikana na hatia ya kumshambulia Mwangalizi wa Ndani wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, Nassir Uronu. 
Hukumu hiyo ilitolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro jana. Hata hivyo, Mbowe alifanikiwa kulipa kiasi hicho cha faini na hivyo kuepuka kwenda kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela. 
Source NIPASHE

0 comments :

 
Top